• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

ARDHI NI HAKI YA KILA MTU

Posted on: December 4th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Kila mtu ambaye ni raia halali wa Tanzania mwenye umri wa miaka kumi na nane  na kuendelea mwenye akili timamu kwa mujibu wa katiba  ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anaruhusiwa kumiliki ardhi. Vigezo vya kugawa ardhi havipaswi kwenda kinyume na katiba ya nchi na haki za binadamu.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akisikiliza na kutatua migogoro ya ardhi katika kijiji cha Chemchem. Ikiwa ni utaratibu aliojiwekea wa kutatua migogoro ya ardhi katika eneo husika lenye migogoro ili kujiridhisha kwa kusikiliza pande zote zenye migogoro.

Mh. Kayanda  amekemea tabia iliyokuwa imejengeka ya serikali ya kijiji cha Chemchem ya kugawa ardhi kwa wananchi kwa kigezo cha mwenye uhitaji lazima awe ameowa. Kipengele hicho amekifuta na ametoa  maelekezo kwa uongozi wa serikali ya kijiji kuhakikisha kila mwenye uhitaji na  aliyekidhi vigezo kuhakikisha analipia ada iliyowekwa na Halmashauri ya kijiji, bila kujali kwamba ni mtoto wa kike au mtoto wa kiume. Ametoa rai kwa vijana wa kijiji cha Chemchem kujitokeza na kujiandikisha  kuomba ardhi ili wafanye shughuli za uzalishaji katika maeneo watakayokuwa wamegawiwa.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa kijiji cha Chemchem wakati akisikiliza kero za wananchi.

Mh. Kayanda ameomba watu kuheshimu jitihada zinazofanywa za kutatua migogoro ya ardhi, amesema kama kuna mtu  anajambo lake na hajaridhika ananafasi ya kwenda kwenye vyombo vya sheria. Amesema ni wakati sasa wa wananchi wa kijiji cha Chemchem kujikita katika shughuli za maendeleo.

Akizungumza kuhusu upataji wa haki kisheria katika migogoro ya ardhi amesema kwa kawaida migogoro yote ya ardhi inaanza kutatuliwa na mabaraza ya ardhi ngazi ya kijiji, inaenda ngazi ya kata, baadae baraza la ardhi na nyumba  ngazi ya wilaya na mahakama kuu kitengo cha ardhi na mwisho ni mahakama ya rufaa. Amesema hizo ni ngazi unaweza kuzifuta kama unaona haki yako hujaipata kwenye upande wa ardhi. 

Katika hatua nyingine Mh. Kayanda amewaambia wananchi wenye malalamiko ya mirathi kuhakikisha wanateuwa msimamizi wa mirathi ili jina lipelekwe mahakama ya mwanzo na liweze kuteuliwa. Amesema hiyo itasaidia msimamizi wa mirathi kuwa na uhalali wa kisheria wa kusimamia malalamiko yake.

Mzee Nicodemus Mwale akizungumza kero yake mbele ya Mkuu wa wilaya ya Karatu

Matangazo

  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE (CSEE) 2020 January 15, 2021
  • MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA KIDATO CHA PILI (FTNA) 2020 January 15, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • WACHIMBAJI WAASWA KUTOJIHUSISHA, UTOROSHAJI WA MADINI

    January 15, 2021
  • UMAKINI WAHITAJIKA UJENZI WA MIUNDO MBINU YA ELIMU

    January 12, 2021
  • VIJANA WAPONGEZWA, KUHITIMU MAFUNZO YA JESHI LA AKIBA

    January 09, 2021
  • ARDHI NI HAKI YA KILA MTU

    December 04, 2020
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0783-577 052

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa