• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

ARUSHA: WAANZISHA KITUO CHA KUSAIDIA WAHANGA WA KIJINSIA

Posted on: June 17th, 2019

Sherehe za siku ya mtoto zimefanyika katika uwanja wa shule ya msingi Endabash. Sherehe hizo zimejumuisha watoto kutoka sehemu mbalimbali katika wilaya ya karatu.Ujumbe wa mkoa kutoka ustawi wa jamii ulitoa taarifa ya matukio ya unyanyasaji wa watoto kwa mkoa wa Arusha.

Ndugu Simoni Panga kamishina wa ustawi wa jamii mkoa amesema, watoto wanapata athari za unyanyasaji wa kihisia, ndoa za utotoni na mimba za utotoni. Amesema mkoa wa Arusha ulikuwa na watoto 54911 wanaoishi mazingira hatarishi na watoto 19421 kati yao wameunganishwa na huduma mbalimbali kama, afya na  elimu ambayo ni sawa na 35%. Bado kuna 65% hawajapata huduma hii ni kwa mujibu wa takwimu za March mwaka huu kutoka kitengo cha ustawi wa jamii mkoa.

Ndugu Simoni amesema kuna mahakama 13 zinazosikiliza mashauri ya watoto mkoa wa Arusha. Mashauri ya watoto 193 yamefikishwa mahakamani kuanzia julay 2018 mpaka march 2019. Jumla ya watu 1437 kwa mwaka (2017-2018) walifanyiwa ukatili wa kijinsia katika mkoa wa Arusha na wahanga wakubwa walikuwa wanawake na watoto, hii ni kwa wale ambao taarifa zao zilifika vituo vya afya na polisi. Ndugu Simoni  amesema wameanzisha kituo cha kutoa huduma kwa wahanga wa kijinsia (one stop centre)  kitengo hicho kimeanza kuanzia mwezi wa tano mwaka huu  hospitali ya Mount Meru Arusha. Ndugu Simoni amesema wahanga wa kijinsia hawahitaji kupata rufaa ili kupata matibabu kwenye kituo hicho.


Ndugu Simoni amesema wamefanikiwa kuwa na kamati ya ulinzi wa mwanamke na mtoto kwa ngazi ya mkoa na kila wilaya. Kamati 506 zimeundwa kati ya kamati 687 sawa na 74%. Ustawi wajamii mkoa wamefuatilia mashauri ya watoto wanaokinzana na sheria kupitia mahakama za watoto zilizoteuliwa na kuna mashauri  ya watoto193 tangu ( Jualai 2018-march 2019 ).

Nalo shirika la world vision limetoa semina katika mabaraza ya watoto katika vijiji 32 vya Tarafa ya Endabash na Eyasi. Ndugu Danile Kirhima amesema wametoa mafunzo ya haki za watoto, na takribani watoto elfu moja walifikiwa katika mafunzo hayo. Mafunzo kwa kamati ya ulinzi wa mtoto na pia yamehusisha viongozi wa dini takribani themanini na viongozi wa jamii na serikali miamoja. Shirika la world vision limetoa elimu pia kwa taasisi zote za elimu, wazazi walimu vijana na wanafunzi. Ndugu Daniel amesema shirika linatoa ushirikiano kwa serikali kuhakikisha watoto wanalindwa na wanaendelezwa ili waweze kufikia malengo yao.

 Ndugu Daniel mratibu wa world vision ametoa raia kwa wazazi, amesema mzazi ndiye mdau wa kwanza  anayeweza kuandaa msingi wa mtoto. Ameomba wazazi kufuatilia mienendo ya watoto wanapokuwa shuleni.


Watoto wakifuatilia jambo wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa Afrika

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa