• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

ASILIMIA ISHIRINI YA MAPATO, IENDE SEKTA YA KILIMO

Posted on: November 5th, 2018

Na Tegemeo Kastus

Naibu waziri wa kilimo Mheshimiwa Omary Mgumba amefanya ziara katika Halmashauri ya Karatu jana. Ziara hiyo ya Naibu Waziri ililenga kujionea shughuli za kilimo na umwagiliaji, na amefanya mkutano kijiji cha Jobaj katika Tarafa ya Eyasi na kusikiliza kero za wananchi.

Mh. Mgumba amesema Halmashauri ya Wilaya ya Karatu inakusanya billion tatu ya mapato. Katika mapato hayo kilimo cha vitunguu kinachangia 29% ya mapato. Mh. Mgumba ameelekeza wananchi kujenga  visima kuvuna maji ya mvua ili yasipotee bure, amewaelekeza wananchi kujiunga na vyama vya ushirika kila kijiji ili waweze kukopesheka na taasisi za kifedha ili waweze kununua zana za kisasa za kilimo.

Mh. Mgumba amesema 20% ya mapato ya Halmashauri yapelekwe kwenye sekta ya kilimo ili iweze kuwasaidi wakulima. Fedha hizo zitumike kama mitaji kwa wakulima, hayo ni maelekezo ya serikali kwa Halmashauri zote. Mhe. Mgumba amesema anafahamu kuna mvutano wa maji ya umwagiliaji kati ya magereza na wananchi. Mh. Mgumba amesema magereza nao wanahitaji maji kwa shughuli zao na kwa ajili kilimo cha umwagiliaji, amesema kuna miradi nane ya maji na mradi mmoja unatumiwa na magereza.

Mh. Mgumba amesema kuna mradi wa utengenezaji wa bwawa la maji la magereza wa miaka 10 iliyopita. Mradi huo umeshindwa kutekelezeka, Mh. Mgumba amesema serikali kupitia wadau wa maendeleo Japan imetoa zaidi ya shilingi 300 millioni lakini bado bwawa halifanyi kazi. Mh. Mgumba amemuelekeza Mkuu wa Wilaya kuunda tume kuchunguza mradi huo.

Mh. Mgumba ametembelea chanzo cha maji na amewaelekeza wananchi kuhifadhi vyanzo vya maji. Amesema kuacha chanzo cha maji wazi kinakauka, Mh. Mgumba ameelekeza wananchi na serikali kupitia Halmashauri waandae miche ya miti na magereza wao wataipanda. Mhe Mgumba amesema ni vizuri wakapanda miti ya matunda ambayo ni rafiki wa maji katika chanzo ili waweze kukilinda chanzo hicho cha maji. Mh. Mgumba amewaelekeza wananchi wanaojishughulisha na kazi za uzalishaji ndani ya mita 60 za chanzo cha maji au mito wanatakiwa kuondoka kwenye vyanzo hivyo vya maji.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa