• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

BARAZA LA WAZEE WILAYA LAZINDULIWA

Posted on: May 1st, 2021

NA TEGEMEO KASTUS

Serikali kwa kutambua umuhimu wa wazee ilitengeneza sera maalumu ya wazee ili kuwashirikisha katika shughuli za uzalishaji mali. Ikiwa ni pamoja na kutoa ulinzi wa wazee na kuboresha huduma zinazotolewa kwa ajili ya wazee kama afya kwa kutoa vitambulisho vya wazee ili wapate matibabu bure. Hatua nyingine muhimu zilizofanywa ni pamoja na kuwaelimisha vijana kutambua na kuheshimu maswala yanayohusu wazee katika jamii.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akizindua baraza la wazee wilaya ya Karatu. Mh. Kayanda amesema wazee ni chanzo muhimu cha habari na wanasaidia sana katika kushauri serikali kutokana na uelewa wao mkubwa wa mambo mengi yanayotuzunguka kwenye jamii. Amesema serikali ilianzisha sera ya wazee ya mwaka 2003 ili kuwashirikisha wazee katika mambo yanayowahusu ili kujua hitaji lao ni nini ??. Ameongeza kusema serikali ilianzisha sera ya wazee ili kuwatambua kama rasilimali muhimu katika maendeleo ya taifa.

Mh. Kayanda amesema umuhimu wa baraza la wazee ni kutengeneza jukwaa la wazee ili waweze kukaa na kubadilishana mawazo n kupeana taarifa juu ya mambo ya wazee ya yanavyokwenda katika jamii. Jukwaa hilo linasaidia kuunganisha wazee na kushauri serikali juu ya mambo mbalimbali kwa kujenga mtizamo sahihi kwa jamii. Amesema baraza la wazee linasaidia wazee kukaa kuzungumza changamoto zao zinazowakabili, na kutoa takwimu sahihi ya idadi ya wazee. Amesema kuwa na takwimu sahihi kunasaidia serikali kujua mahitaji sahihi yanayohitajika katika kundi la wazee. Amesema wazee waliopewa nafasi ya kuunda baraza la wazee watasaidia sana serikali katika mambo ya ulinzi na usalama.Mh. Kayanda ametoa rai kwa baraza la wazee kuwa sehemu ya matokeo chanya badala ya kuwa chombo cha kukinzana na serikali.

Mh. Abbas Kayanda (kushoto) akipokea kibao ambacho ataweka kwenye ofisi yake katika ufunguzi wa baraza la wazee wilaya ya Karatu.

Katibu wa baraza la wazee wilaya ya Karatu Daudi Askwari amesema baraza la wazee la wilaya limeundwa na wajumbe wazee saba.  Baraza la wazee limeundwa kuanzia January mwaka 2021ili kuwakilisha wazee katika vikao vya maamuzi. Mzee Askwari amesema baraza la wazee litahimiza umoja na mshikamano kwa jamii na mpango wao ni kufanya uzinduzi wa mabaraza ya wazee katika ngazi ya vitongoji, vijiji na kata.

Mzee Askwari amesema ratiba ya uzinduzi  itaanzia  tarehe 1 -15 mwezi 5 mwaka 2021 mabaraza ya kata ambayo  yatakuwa yamezinduliwa. Tarehe 16-17 mwezi june mabaraza ya wazee ya wazee ya vijiji na vitongoji yatakuwa yamezinduliwa. Amesema wawakilishi katika ngazi ya kitongoji vijiji na kata wanatakiwa kushiriki katika vikao vya maamuzi.  Amesema wamefarijika kuona wawakilishi wa baraza la wazee la wilaya tayari wameanza kuwakilisha wazee kwenye baraza la madiwani.


Mwenyekiti wa Halmashauri Mh. John Lucian (kushoto) akipokea kibao atakachoweka kwenye ofisi yake.

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu Ndg. Waziri Mourice (kushoto) akipokea kibao atakachoweka kwenye ofisi yake

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa