NA TEGEMEO KASTUS
Fidia kwa ajili ya wananchi waliopisha utanuzi wa uwanja wa ndege wa Manyara, Karatu ipo katika hatua za mwisho kukamilika kwake ili wananchi walipwe fedha zao. Kilichobakia ni taarifa ya uthamini kusainiwa ili kwenda kwa Mthamini Mkuu wa serikali Dodoma na baadae taarifa hiyo kupelekwa Tanroad.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Kilimamoja. Amesema serikali haina dhamira ya kuchelewesha malipo kwa wananchi, Mh.Kayanda amesema kabla ya mwaka huu kuisha wananchi watakuwa wameshalipwa fidia zao. kiasi cha billion tano kitatolewa na serikali kwa ajili ya kuwafidia wananchi. Lakini kabla ya fedha hizo kutoka kuna taratibu zinapaswa kufuatwa na zikamilike ili fedha hiyo ya fidia kwa wananchi iweze kutolewa, Mh. Kayanda ameomba wananchi kuvuta subira ili uwasilishaji wa taarifa ya uthamini ukamilike, amesema swala hilo analifuatilia kwa karibu hatua kwa hatua. Wakati huo huo Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi kwa mtendaji wa kijiji cha chemchem kusitisha zoezi la ugawaji wa viwanja katika kijiji cha chemchem mpaka maelekezo mengine yatakapotolewa.
Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa kijiji cha kilimamoja.
Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi pia kwa viongozi wa kijiji cha Kilimamoja kusimamia na kuhakikisha ujenzi wa machinjio ya Kilimamoja unakamilika tarehe 10 mwezi wa tisa kama walivyojipangia. Lakini kuhakikisha ujenzi wa jengo la machinjio unaendana na thamani ya fedha iliyotolewa, Halmashauri imetoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa machinjio ya Kilimamoja hivyo ni jukumu la viongozi kusimamia ujenzi wa machinjio na kukamilika. Huduma za kuchinja mifugo katika kijiji cha kilimamoja kwa sasa zinafanyika Makuyuni.
Sambamba na hilo Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi kwa viongozi wa kijiji kusimamia ujenzi wa zahanati katika kijiji cha Kilimamoja ili baadae serikali iongeze nguvu za kumalizia.Wananchi wa kijiji cha kilimamoja walishaanza ujenzi wa Msingi wa zahanati, amesema wananchi lazima wawe chachu ya kuibua miradi ya maendeleo na kuchangia shughuli za maendeleo.
Wananchi wa kijiji cha kilimamoja wakimsikilza Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. AbbasKayanda ( aliyesimama kulia) akihutubia
Mh. Kayanda ameelekeza uongozi wa maji kijiji cha Kilimamoja kuhakikisha wananchi wanapata maji. Amesema viongozi wa maji wamepewa dhamana ya kusimamia na kuhakikisha wananchi wanapata huduma ya maji katika maeneo yao bila usumbufu. Mh, kayanda ametoa wito kwa wananchi kulipa bili za maji kwa wakati ili kusaidia usambazaji wa huduma za maji. Fedha hizo husaidia viongozi wa maji kufanya ukarabati wa miundo mbinu pindi inapotokea hitilafu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa