• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

BUSARA KUTUMIKA KUTATUA MGOGORO WA ARDHI KAMBI YA SIMBA

Posted on: January 31st, 2019

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo leo amefanya mkutano wa hadhara na wananchi wa Kambi ya Simba. Katika mkutano huo Mhe. Theresia Mahongo amewaomba wananchi wa kijiji cha Kambi ya Simba kuendelea kutunza amani.

Katika mkutano huo Mhe. Theresia Mahongo alipata nafasi ya kusikiliza pande zinazovutana juu ya sehemu ya ardhi ambayo Chama cha Ushirika Kambi ya Simba kinailalamikia Halmashauri serikali ya kijiji cha Kambi ya Simba kwa kutwaa ardhi yao.

Mhe. Theresia Mahongo amesema ndani ya muda wa wiki mbili mvutano wa Chama cha Ushirika Kambi ya Simba na serikali ya kijiji cha Kambi ya Simba juu ya uhalali wa eneo linalomilikiwa Chama Cha Ushirika utapatiwa ufumbuzi. Mhe. Theresia amesema busara itatumika kutatua mvutano huo, amesema chama cha ushirka ni chetu na kijiji pia ni chetu.

Mhe. Theresia amesema serikali inataka kuimarisha Vyama Vya Ushirika, amehimiza wananchi kujiunga kwenye Chama Cha Ushirika. Amesema ushirika sio wa watu wachache, jambo la msingi ni kufuata taratibu za kujiunga na Chama Cha Ushirika, ameomba wananchi kutoa taarifa kama kuna mtu anawakataza watu wasiingie kwenye Chama Cha Ushirika. Mhe. Theresia ameshangazwa na chama cha Ushirika kuwa na wanaushirika arobaini tuu na ameahidi kulifuatilia kwa undani kwanini watu hawajiungi na Chama Cha Ushirika.

Mhe. Theresia amewahimiza wananchi kuwapeleka watoto shule, amesema kamata kamata kwa wazazi ambao watashindwa kupeleka watoto shule itaanza. Amewaomba wananchi kuwapatia watoto chakula wanapokuwa shuleni. Mhe. Theresia amesikitishwa na ufaulu duni wa wanafunzi katika mtihani wa kidato cha nne. Mhe. Theresia amewahimiza wazazi kuwaendeleza masomo ya ufundi watoto ambao hawakufanya vizuri katika mitihani yao ya mwisho katika chuo cha Veta.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa