• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

DC AFANYA UKAGUZI WA ENEO LA MNADA NA SOKO

Posted on: August 6th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Wajumbe wa kamati ya ulinzi na usalama wakiongozwa na mkuu wa wilaya ya Karatu wamefanya ziara katika eneo la mnadani Karatu. Wametembelea na kuona eneo la machinjio ya mnadani na eneo lilojengwa choo cha umma kinachosimamiwa na Halmashauri.

Mh. Abbas Kayanda Mkuu wa wilaya ya Karatu ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Karatu kuhakikisha milango na madirisha ambayo imeharibiwa na kuibiwa katika maliwato hayo yanarudishwa  na kuwekwa ifikapo tarehe 24 mwezi wa nane mwaka huu. Mh.  Kayanda ameelekeza miundo mbinu ya maji ambayo nayo ilikuwa imeondolewa ikarabatiwe na kuwekwa katika Maliwato hayo. 

Hali ya vioo vya madirisha ilivyo katika maliwato hayo baada ya kuvunjwa  na milango kung'olewa

Mh. Kayanda amesema lazima mali  zote za umma zitunze na kulindwa, amekemea uzembe uliofanywa katika jengo hilo la maliwato baada kwa kukosa Mlinzi anayelinda Maliwato ya eneo hilo, jambo lilotoa mwanya kwa watu wasio waaminifu kuvunja madirisha na kuiba milango ya maliwato yaliyojengwa katika eneo hilo la mnada.  Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji kurekebishwa miundo mbinu ya Machinjio ya mnadani na kuliweka eneo hilo katika mazingira ya usafi pamoja na kulinda miundo mbinu ya machinjio.

Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa Afisa mazingira kuhakikisha mji wa Karatu unakuwa msafi, amesema bado katika swala la usafi Karatu tupo nyuma. Watu wanatupa taka hovyo amesema lazima usafi usimamiwe ili  siku moja tuwe mfano wa Halmashauri zenye mazingira safi hasa ukizingatia mji wa Karatu ni mji wa kitalii.

Mh. Kayanda ametembelea eneo la soko kuu la mjini wa Karatu ambalo ujenzi wa vizimba 202 unaendelea kwa awamu. Pamoja na eneo la mbele ambalo limeachwa kwa ajili ya ujenzi wa maduka. Mh. Kayanda ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri kuhakikisha ujenzi huo unakamilika haraka na kwa wakati ili wakati vizimba vya kwanza vianamaliziwa kuwekwa plasta vizimba vilivyobakia vianze kujengwa ili wananchi waanze kulitumia soko mapema iwezekanavyo. Mh. Kayanda ametoa ameelekeza miundo mbinu ya umeme iwe tayari kabla wafanyabiashara hawajaanza kuingia na kulitumia soko.

Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda akikagua maendeleo ya ujenzi wa Vizimba katika eneo la soko kuu Karatu.

Mh. Kayanda ametembelea jengo la Halmashauri la zamani ambalo awali lilikuwa halijafanyiwa ukarabati kwa muda mrefu. Mh. Kayanda ameona jengo hilo likiwa limefanyiwa ukarabati wa ofisi pamoja na samani za ofisi zikiwa katika hali nzuri na limekuwa tayari kutumiwa kama ofis ya Afisa mamlaka ya mji mdogo wa Karatu. Mh .kayanda amepongeza Mkurugenzi Mtendaji kwa ukarabati Mzuri  amemuelekeza  Afisa Mji mdogo  wa Karatu pamoja na wafanyakazi  wa mamlaka ya mji mdogo kulitumia na kuendelea kutunza miundo mbinu ya  jengo pamoja na samani zilizopo katika jengo hilo.


Mkuu wa wilaya ya Karatu. Mh. Abbas Kayanda akikagua Ukarabati wa Ofis ya Mamaka ya Mji mdogo Karatu. 

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa