NA TEGEMEO KASTUS
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh.Abbas kayanda amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa shrikisho la mpira wa miguu Tanzania ndg. Walles Karia pamoja na viongozi wengine wa TFF.
Mazungumzo hayo yalijikita katika kupambanua namna bora za kuendeleza mpira wa miguu wilayani Karatu. Lakini pia namna ya kuibua vipaji vipya vya vijana na kuendeleza kukuza sekta ya mpira wa miguu wilayani Karatu. Mh. Kayanda pamoja na viongozi wa TFF walipata nafasi ya kutembelea uwanja wa kisasa wa michezo uliojengwa na Mtanzania Mzalendo ndg. Nikson Mkurugenzi wa Black rhino International school.
Mh. Abbas Kayanda pamoja na rais wa TFF walipotembelea uwanja wa kisasa wa mpira uliojengwa na Ndg. Nikson katika shule ya Black Rhino International school.
Mh. Abba kayanda akiwa katika pamoja na Rais Ndg.Karia na viongozi wengine wa shirikisho la mpira wa miguu tanzania.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa