• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

DKT, MUSTAFA: WANANCHI JITOKEZENI KUJIANDIKISHA ICHF

Posted on: June 21st, 2019

Mganga mkuu wa wilaya Dkt. Mustafa Waziri amewaomba wakazi wa Karatu wajitokeze kwa wingi kujiandikisha katika bima ya afya iliyoboreshwa. Ni vyema watu wakawa na bima kwa sababu itasaidia kuboresha upatikanaji wa dawa, na kuviboresha zaidi vituo vya afya na zahanati kupitia mfuko huo wa bima ya afya iliyoboreshwa ICHF.

Dkt Mustafa amesema Karatu ni wilaya kwanza kuanza mfumo wa bima ya afya iliyoboreshwa ICHF kwa Mkoa wa Arusha. Amesema kwa sasa Karatu imeshanunua simu 32 kwa kila kituo na zitahudumia vijiji vyote 57 vya Karatu kupitia waandikishaji wa bima ya afya. Bima hii imeboreshwa kwa sababu mgonjwa anaweza kuhamishwa (referal) kutoka kituo kimoja kwenda kingine kwa ajili ya kupata huduma nzuri zaidi. Dkt Mustafa amesema kazi za simu ni kwa ajili ya upigaji wa picha kwa wanachama wa ICHF na utumaji wa taarifa na mapato ya fedha kwenye mfumo.

Dkt. Mustafa ametoa wito wananchi kujitokeza kujiandikisha kwenye mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. Amesema binadamu huwezi kufahamu ni wakati gani unaweza kuugua na kama una fedha au hauna. Dkt.Mustafa amesema ukiwa na bima ya afya iliyoboreshwa inakuwa msaada kwa mwananchi. Bima hii inawezesha wananchi kulipia shilingi 30000 kwa watu sita na kupata huduma ya afya badala ya kutumia mfumo wa malipo ya hapo kwa hapo. Dkt  Mustafa amesema Karatu ina wanachi takribani 245000, wananchi wengi wakijitokeza kujiandikisha  ili kupata ICHF iliyoboreshwa vituo vya afya vitaimarika zaidi kwa kupata dawa. Fedha za mfuko huo 50% zitatumika kununua dawa  katika vituo vya afya lakini pia kuimarisha  miundo mbinu ya maji na umeme katika vituo hivyo.

Ndugu  Ahmadi Masudi Mratibu wa ICHF wilaya akisisitiza jambo kwa wasimamizi wa ICHF

Dkt Mustafa amesema mwamko wa wananchi kwa ajili ya uandikishaji wa bima ya afya ni mkubwa ila taratibu za kiserikali kwa ajili ya uandikishaji zilikuwa hazijakamilika  lakini hivi sasa taratibu zimekamilika kwa ajili ya uandikishaji wananchi kwa ajili ya mfumo wa bima ya afya ICHF. Amesema Upatikanaji wa dawa kwa mwaka 2018 ulikuwa kwa 92.2% amesema kwa mwaka 2019 upatikanaji wa dawa ni 97.9%. Dkt. Mustafa amesema changamoto ya dawa ilikuwa kipindi cha nyuma lakini kwa sasa hakuna changamoto ya upatikanaji wa dawa.

Mratibu wa ICHF iliyoboreshwa ndugu Ahmadi Masudi amesema muitikio wa wananchi  katika ICHF  utakuwa mkubwa. Ndugu Ahmadi amesema kuongeza wigo wa kupata matibabu kwa mgonjwa baada kupata idhini (referal) ya kupata matibabu kufikia ngazi mkoa ni jambo litakalowavuta wananchi wengi kujiunga katika mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa. Ndugu Ahmadi  amesema CHF ya zamani iliweza kuandikisha wananchi wa Karatu  kwa 31% amesema wanatarajia kuandikisha wananchi zaidi  50% iliyowekwa kisera.

Ndugu Masudi amesema Halmashauri imepita katika hatua tatu kufikia kutoa semina ya uelewa kwa wasimamizi wa ICHF. Hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwapata waandikishaji wa ICHF lakini hatua ya pili ilikuwa kununua simu na sasa ni semina ya  uelewa kwa wasimamizi wa ICHF.



Wasimamizi wa ICHF katika semina.


Wasimamizi wa ICHF wakifuatilia semina kwa Umakini.

Wasimamizi wa ICHF katika matukio Mbalimbali

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa