Mhe. Mkuu wa wilaya ya Karatu amefanya kikao na wananchi wa kijiji cha Laja na kusikiliza kero zao zinazo wasumbua. Katika mkutano huo na wananchi umehudhuriwa na watendaji kutoka Wilayani, wajumbe wa serikali ya kijiji na wananchi ambao wametoa kadhia na dukuduku kwa mambo mbalimbali yanayowasumbua na hatimae kujadiliwa katika mkutano.
Mhe. Theresia amemuagiza Mtendaji wa kata ya Kansay kusimamia na kutatua mgogoro wa ardhi wa ndugu Nikodemus Yona. Aliyedai katika kikao hicho eneo la familia kiasi cha hekari sita limechukuliwa na mtu anayedai kwamba aliuziwa na mmoja wa wanafamilia kwa kupewa pombe. Mhe. Theresia amesikiliza malalamiko ya mwananchi huyo na amesema haiwezekani eneo lenye ukubwa wa hekari takribani sita kuuzwa kwa pombe. Amemuelekeza mtendaji wa kata kukutanisha pande zote zinazoshitumiana katika mgogoro wa sehemu hiyo ya ardhi ili tatizo hilo liweze kupatiwa ufumbuzi. Mhe Theresia amemuelekeza ndugu Elikana Lukasi, kupeleka hati za umiliki wa eneo hilo katika ofisi ya Mkuu wa wilaya ifikapo Alhamisi, wakati shauri linalolalamikwa likiendelea kusuluhishwa katika ngazi ya baraza la kata.
wananchi wakiwa katika Mkutano kijiji cha Laja.
Ndugu Nikodemus Yona ambaye ni malalamikaji wa eneo lililotwaliwa na Ndugu Elikana Lukasi amesema kwenye mkutano huo kwamba wanaonewa. Ndugu Nikodemus anasema eneo hilo lilitwaliwa baada ya baba mwenye eneo hilo kufungwa. Anasema kutokana na ugumu wa maisha, mama aliyekuwa analimiliki eneo hilo ambaye ni mke wa mzee aliyefugwa aliondoka katika eneo hilo na vijana wake wa tatu. ameongeza kusema mama aliyekuwa anamiliki eneo hilo hakuwa sawa kiakili alipondoka na watoto wake, ndugu Elikana Lukasi ambaye ni jirani katika eneo husika alitumia mwanya huo kulivamia eneo hilo na kuanza kulijenga. Anasema sasa mama huyo amerudi na watoto wake ambao washakuwa wakubwa na wanataka kujenga kwenye eneo lao. Ndugu Nikodemus amesema wamefika ofisi ya kijiji ili kuomba suluhu ya eneo la heka sita na robo tatu linalodaiwa kuuzwa kwa magunia matatu na pombe. Ameongeza kusema awali waliomba ofisi ya kijiji kuridhia mgogoro huo usikilizwe na wazee wa kijiji. Ndugu Nikodemus amesema uongozi wa kijiji iliridhia mgogoro huo kusikilizwa na wazee wa kijiji ili kupata muafaka lakini mudaiwa alikataa kuitikia wito wa kusikiliza lalamiko ya mgogoro huo wa ardhi. Ndugu Nikodemus amesema ilimlazimu kwenda ofisi ya kata na kutoa malalamiko na kumuita mulalamikiwa ambaye aliitikia wito na kutoa hati ambazo anadai aliuziwa kwa shilingi million nane mwaka 1994. Lakini alipoombwa na Mlalamikaji ili kupitia hati hizo wathibitishe uhalali wake, mdaiwa aligoma. Mdaiwa aligoma kutoa mutasari wa mauziano ya eneo hilo pia ili walalamikaji wajiridhishe. Ndugu Nicodemus amesema hali hiyo ilimfanya kwenda ofisi ya mkuu wa wilaya ambayo msaidizi wa ofisi alimuagiza katibu Tarafa kusimamia tatizo hilo. Ndugu Nikodemus amesema baada ya kuwasiliana na katibu Tarafa alimuelekeza kwenda kwa mtendaji wa kata . amesema baada ya kurudi tena kwa mtendaji wa kata mlalamikiwa ndugu Elikana hakuonesha tena hati alizodai aliuziwa, badala yake akasema alipewa shamba hilo baada ya kumpa baba mmiliki wa shamba Pombe.
Wananchi wakifuatili Mkutano
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa