• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MHE.GEJE, AUKWAA, UENYEKITI WA HALMASHAURI

Posted on: September 3rd, 2019

Mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya Karatu umeendelea kwa siku ya pili, ambayo baraza limetumia kuchagua Mwenyekiti mpya wa Halmashauri. Nafasi ambayo ilibaki wazi baada ya aliyekuwa Mwenyekiti kuondolewa kwenye nafasi katika kikao maalum cha baraza la madiwani.

Kikao cha uchaguzi kiliongozwa na ndugu Abbas Kayanda kwa  mujibu wa kanuni za Halmashauri namba 6 kifungu cha pili inayoelekeza utaratibu wa kufuata kuijaza nafasi ya mwenyekiti kwa muda, pindi baraza linapokuwa halina Mwenyekiti Halmashauri wala Makamu mwenyekiti.  Ndugu Waziri Mourice katibu wa baraza alitangaza majina ya wagombea ambayo ni Mhe. Lazaro Bajuta kutoka kata ya Ganako na Mhe. Lazaro Geje Kutoka kata ya Mang’ola na wagombea wote walitoka chama cha mapinduzi ambacho ndio chama pekee kilichotoa majina ya wagombea wa   nafasi hizo mbili.

Mwenyekiti wa muda wa kikao ndugu Abbas Kayanda alitangaza mshindi wa nafasi ya Mwenyekiti mpya wa Halmashauri kuwa ni Mhe.Lazaro Geje. Mhe. Geje alipata ushindi wa kura 15 kati ya kura 3 zilizomkataa. Mwenyekiti ndugu Abbas alisema kwa mamlaka aliyopewa kwa ya kanuni ya 6 kifungu cha pili namtangaza Mhe. Geje kuwa Mwenyekiti mpya wa Halmashauri. Baraza hilo lilimchagua Mhe. Lazaro Bajuta kuwa Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo amewahusia viongozi wateule kuwa makini katika utendaji wa kazi zao ili wasiwaumize wananchi. Amesema kutenda kazi vizuri ni kutekeleza yale mliowaahidi wananchi, ambao wamewaamini na kuwateuwa. Mhe. Theresia amewaelekeza viongozi walioteuliwa kusimamia vizuri mapato ya ndani ya Halmashauri na kuepuka hoja za ukaguzi za mara kwa mara zinazokwamisha maendeleo ya wilaya.

Naye Katibu Tawala wa wilaya  ndugu Abbas Kayanda  amempongeza Mwenyekiti Mpya wa Halmashauri na Makamu mwenyekiti kwa kuteuliwa kushika nafasi hizo. Amesema wananchi wanataka mabadiliko, kutoka sehemu waliyopo na kwenda mbele zaidi kimaendeleo. Ndugu Abbas amewaahidi Mwenyekiti wa Halmashauri na Makamu mwenyekiti, kwamba watapata ushirikiano mzuri  kutoka kwa watendaji wa Halmashauri.

Kikao hicho cha baraza la madiwani kilitumika kujaza nafasi za wenyeviti wa kamati za Halmashauri, baada ya wenyeviti wa awali kuhama vyama vyao na kuacha nafasi hizo wazi. Mhe, Yotham Manda ameteuliwa kuwa mwenyekiti wa kamati ya elimu maji na afya. Mhe. Josephat Margwe ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya uchumi.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa