Na Tegemeo Kastus
Mdau wa elimu Ndugu Elias Philip Simpa, jana ametoa vifaa vya elimu vyenye thamani ya shilingi 300,000 kwa shule ya sekondari Awet, kata ya Mbulumbulu. Vifaa hivyo ni madaftari makubwa, mathematical set na mbuzi ili kuhamasisha shughuli za michezo shughuli za kitaaluma.
Ndugu Simpa ametoa daftari kubwa tatu na mathematical set kwa kila mtoto aliyeshika nafasi ya kwanza, daftari mbili kwa mtoto aliyeshika nafasi ya pili na daftari moja kwa mtoto aliyeshika nafasi ya tatu, zawadi hizo zimetolewa kwa kidato cha kwanza mpaka cha nne.
Ndugu simpa amehimiza jitihada kwa wazazi na walimu, amesema shule ya sekondari Awet ni shule Kongwe katika kata ya Mbulumbulu, tunahitaji kuwekeza kwenye elimu ili tupande kitaaluma. Kazi ya walimu ni kuelekeza wanafunzi hatuna budi kuondoa daraja la nne na sifuri. Bila taifa lenye elimu taifa litakuwa gizani, bila kusoma uchumi wa viwanda hatuwezi kuufikia, nyie wanafunzi ndio mtakao chukua nafasi zetu.
Ndugu Simpa amehimiza wanafunzi kupenda masomo ya sayansi na ameahidi kutoa shilingi 50000 kwa kila mwanafunzi atakaye faulu mtihani wa kuhitimu kidato cha nne kwa kiwango cha daraja la kwanza. Nidhamu zuri inahitajika kwa wanafunzi ili waweze kufanya vizuri katika masomo.
Ndugu Simpa ametoa zawadi ya mbuzi kwa mshindi wa ligi ya mbuzi iliyofanyika katika shule hiyo ya sekondari Awet. Pia ametoa zawadi kwa mfungaji bora wa mashindano hayo, mchezaji bora wa mashindano, waamuzi waliochezesha michezo sambamba na makocha.
Mwalimu mkuu wa shule ya sekondari Awet Ndugu Christopher Sulle, amemshukuru Ndugu Simpa kwa mchango wake amefurahia zawadi hizo amesema swala la taaluma linamgusa kila mtu, ameesema Ndugu Simpa amejinyima ili kusaidia elimu huu ni mwanzo mzuri.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa