• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

HOJA ZILIZOKUWA KAA LA MOTO HALMASHAURI, ZAPATA UFUMBUZI

Posted on: July 16th, 2019

Kikao maalum cha baraza la madiwani kwa ajili ya kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa serikali ya hesabu za Halmashauri za mwaka wa fedha ulioisha tarehe 30/june/2018 kimefanyika katika ukumbi wa Halmashauri  ya wilaya ya Karatu.

Mkuu wa Mkoa Mhe. Mrisho Gambo amepongeza wataalamu wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu kwa kupata hati safi. Amempongeza sana Mkaguzi mkuu wa serikali kwa kazi nzuri aliyoifanya, na kubaini matatizo mbalimbali. Amesema ameagiza Halmashauri zote wapate  taarifa  za kibanki; Manunuzi, kwa Mkaguzi wa ndani, mara baaada ya kukamilisha mabaraza yote mkoa mzima, ili kwa kushirikiana na Menejimenti ya mkoa ziweze kufuatiliwa. Amesema taarifa hizo pia zitasaidia kufanya mlinganisho kwa kushirikisha wakaguzi wa serikali ili kuongeza umakini na kuondoa kutojiruadia kwa dosari zilizojitokeza. Amesema hoja nyingi za Halmashauri inazopata ni uzembe, inawezekana vikao vya maamuzi vya Halmashauri havifanyi kazi vizuri au kamati ya fedha ya Halmashauri haifanyi kazi vizuri. Amesema ni imani makosa ya namna hii hayatajirudia tena, na dosari zilizojitokeza zitapatiwa ufumbuzi kwa wakati.

Awali katika kikao hicho hoja ya vifaa vya ujenzi vilivyolipiwa lakini havikuwasilishwa Halmashauri vienye thamani ya sh.79,542,000 uliohusisha Msambazaji Anatoly construction ilibainika wakati wa ukaguzi uliofanywa na mkaguzi mkuu wa serikali.  Ushauri wa mkaguzi Mkuu wa serikali kwa Halmasahuri ilikuwa kuimarisha uthibiti wa mifumo yake na pia fedha yote inayolipwa kwa mzabuni irudishwe kwa Halmashauri. Hivyo kamati iliona kuna udhaifu katika manunuzi ya umma. Hivyo Mhusika wa kitengo cha manunuzi kuandikiwa barua ya onyo yenye kumbukumbu na. KDC/DED/Cs.1/8/VOL.1V/30 na ilielekezwa kufuata sheria za manunuzi ili kuzuia hoja kama hizo. Hatua hizo zlichukuliwa baada ya kamati ya ukaguzi kubaini vifaa  ambavyo vimeshalipiwa kutoletwa kwa ajili kukamilisha ujenzi wa soko.

Awali kamati ya fedha ilijadili hoja hiyo na kutoa maamuzi baaada wiki moja vifaa vilivyokuwa vimekosekana viwe vimeletwa na kuweka stoo, lakini mpaka kikao kinafanyika vifaa havikuwa vimeletwa stoo.  Mkurugenzi mtendaji ndugu Waziri Mourice ambaye alikuwa Khatibu wa kikao hicho, alikiri udhaifu katika utendaji wa kulishughulikia swala hilo. Amesema ndani ya wiki moja vifaa vyote vitakuwa vimeshaletwa kutoka kwa msambazaji, na kamati ya fedha ya Halmashauri itapitia kuhakiki vifaa hivyo.

Kaimu mkaguzi wa nje ya Mkoa Monica Mushi amesema swala hilo linaleta utata baada ya kitengo cha manunuzi kutoa fedha zote kwa ajili ya kununua vifaa kwa muuzaji. Amesema ilitarajiwa baada ya kutoa kiasi chote cha fedha vifaa viletwe vyote lakini kitendo cha kununua halafu unaacha vifaa kwa msambazaji, sisahihi kwa sababu anaweza kukataa kwa kusema ameshakuuzia na hana vifaa hivyo tena. Amesema udhaifu wa kuonesha vifaa vimenunuliwa kwenye nyaraka halafu vifaa vikaachwa kule ndio unaoleta hoja. Amesisitiza siyo lazima kulipa fedha nyingi katika kununua vifaa vyote,  bado tunaweza kununua vifaa kidogo kidogo kadri ya mahitaji.

Hoja nyingine ambayo ilileta mjadala kwa Halamashauri wakati wa kikao ilikuwa, ni mapungufu ya katika usimamizi wa vibanda vilivyo katika eneo la mnada. Mkaguzi wa serikali alibaini vibanda hivyo kushindwa kukamilika kwa wakati, lakini pia kiwanja kugawiwa kwa zaidi ya mtu mmoja na kwa watu ambao hawakuwa kwenye orodha. Mkaguzi wa serikali alibaini baadhi ya wapangaji wa  vibanda wamemilikishwa na kugawiwa  watu wengine bila kuwa na makubaliano na Halmashauri.

Menejimenti ya Halmashauri katika majibu yake kwa mkaguzi ilisema kulikuwa na makosa ya ya uhandisi kujirudia  kwa majina na ramani na mikataba ya wamiliki. Hivyo uhakiki unaendeelea ili kuondoa tatizo la majina ya wamiliki kujirudia. Menejimenti ya Halmashauri imedai waliopewa vibanda walipewa kutokana na maombi ya malipo yaliyofanyika baada ya kupata vibanda. Menejimenti ya halmashauri imedai mkataba haumruhusu mmiliki kumilikisha mtu mwingine bila makubaliano ya Halmashauri.

Baraza limeamua  watu waliopewa vibanda na kujenga mpaka kwenye hatua ya kuweka paa na watu walioanza kujenga msingi wapewe muda ili waweze kukamilisha ujenzi wa vibanda hivyo. Baraza limebaini vibanda 109 viko katika hatua ya kuweka paa, na wamepewa muda wa mwezi mmoja wawe wamemaliza kujenga vibanda hivyo. Vibanda 323 viko katika hatua ya kujenga msingi baraza limeamua kuwapa muda wa miezi miwili kumaliza ujenzi wa vibanda hivyo. Baraza limeamua wamiliki wa vibanda 122 ambao hawajaendeleza wanyang’anywe umiliki wa vibanda hivyo.  

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa