Mkuu wa mkoa wa Arusha amehitimisha ziara yake ya siku tano wilayani Karatu, kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo pamoja na kuzungumza na kutatua kero za wananchi. Mkuu wa mkoa ametembelea pia mradi wa muwekezaji binafsi aliyejenga hotel ya kitalii Ngorongoro Coffee Lodge.
Mhe. Mrisho Gambo amesema mkoa wa Arusha unategemea sana wilaya ya Karatu katika shughuli za utalii. Amesema Karatu ni wilaya ambayo inahotel nyingi kuliko wilaya zote za mkoa wa Arusha. Amesema Rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzani Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli alipokutana na mabalozi wanaowakilisha nchi zao Tanzania mwezi January mwaka huu, alisema mwaka 2019 ni mwaka wa uwekezaji. Amesema Mhe. Rais alitaka viongozi wa ngazi za mkoa na wilaya kuhakikisha wanashirikiana na wafanyabiashara na wadau wote ili wapate mazingira mazuri zaidi ya kuwekeza.
Mhe. Gambo amesema amefurahi kuona muwekezaji mzawa anajenga hoteli kwa ajili ya kuwapokea watalii. Amesema kwa mujibu wa wizara ya maliasili na utalii bado Tanzania ina hotel chache, Mhe. Gambo amempongeza mkuu wa wilaya ya Karatu kwa kuhamasisha wawekezaji kuwekeza kwenye maswala ya utalii na hotel ambazo ni sehemu ya maelekezo ya serikali. Mkuu wa mkoa amempongeza bwana Jackobo Hombay kwa uwekezaji, amesema serikali inatambua uwekezaji wake ambao umetoa fursa kwa wanachi kupata ajira. Amesema kupitia maradi huo serikali itajipatia kodi lakini pia utachochea uchumi.
Mhe. Gambo amesema swala la ulinzi na usalama ni swala muhimu sana katika maendeleo ya utalii. Amesema wao kama viongozi watasimamia na kuhakikisha ulinzi na usalama unakuwepo, ili kupitia fursa ya utalii tuweze kuuza bidhaa nyingine za utalii.
Muonekano wa nje wa Ngorongoro coffee Lodge
Muwekezaji ndugu Jackobo Hombay ambaye amejenga hoteli hiyo kwa ushirikiano na muwekezaji mwenzake Reginald. Amesema alianza kazi zake za biashara miaka ya 70 kwa kufungua mgahawa na baadae hoteli ndogo ya kawaida na baadae biashara ikakua na kufika kwenye uwekezaji mkubwa.
Mwekezaji Jackobo amesema hotel ndio kwanza imeanza kufanya kazi, na uwekezaji wa hoteli hiyo umegharimu takribani billion tatu. Amesema kwa sasa wameajiri wafanyakazi thelathini na tano na malengo yao ni kuajiri wafanyakazi zaidi ya hamsini. Ndugu Jackobo ameomba serikali kuzidi kuwaunga mkono kwa kuhakikisha usalama na utulivu unakuwepo ili watalii waweze kuja kwa wingi nchini.
Mwekezji Jackobo amesema siri kubwa ya mafanikio ni kuthubutu kutenda, bila kuwa na uthubutu hakuna jambo linalowezekana. Amesema hata uwekezaji wake wa hoteli ameweza baada ya kukopa fedha. Amesema hotel ina vyumba vya kisasa na vina mabafu matatu, bafu ya kawaida bafu ya nje na bathtub. Amesema kuna unafuu wa gharama kwa wenyeji ukilinganisha na raia wa kigeni na bei hizo hutofautiana kutokana na msimu , kuna kipindi watalii wanakuja kwa wingi (high season) na msimu watalii wanakuja kidogo. Wilaya ya Karatu ina hotel zenye nyota moja mpaka nyota tano kwa ujumla hamsini na nane kwa sasa.
Mhe. Mrisho Gambo akipewa maelekezo na muwekezaji wa Hotel ambaye kwenye picha hayupo katika moja ya jengo la Hotel
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa