Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Ndg. Juma Hokororo leo Mei 12, 2025 amewapokea Madaktari bingwa walioko chini ya mpango wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan awamu ya Tatu waliofika karatu kwaajili ya kutoa huduma za afya kwa wananchi kwa gharama nafuu.
Madaktari hao Bingwa wamewela Kambi hospitali ya Wilaya kwanzia leo leo 12 Mei 2025 na inatarajiwa kudumu kwa siku sita.
Huduma zinazotolewa na madaktari hawa bingwa ni pamoja na
- Huduma za afya kwa watoto na watoto wachanga
- Huduma za afya ya uzazi, wajawazito na magonjwa ya wanawake
-Huduma za magonjwa ya ndani kama shinikizo la damu na kisukari
- Huduma za upasuaji
- Huduma za ganzi na usingizi
Huduma hizi zinalenga kuwafikia wananchi wengi, hasa wale wa maeneo ya vijijini, na zinatolewa kwa gharama nafuu huku Bima ya Afya ya itatumika .
Mpango huu ni sehemu ya juhudi za serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan katika kusogeza huduma za kibingwa karibu na wananchi wote, bila kujali mahali walipo. Wananchi wote wanahimizwa kujitokeza kwa wingi kupata huduma hizi muhimu.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa