Mwenge wa uhuru umezindua mradi wa maji kijiji cha Ayalaliyo, Mradi huo umegharimu jumla ya Tshs 226,239,520/=, kati ya fedha hizo Shirika la World Vision Tanzania walichangia kiasi cha Tshs 206,169,070/=, Serikali Kuu ilichangia kiasi cha Tshs 9,870,450 na Wananchi walichangia nguvu kazi zenye thamani ya kiasi cha Tshs 10,200,000.
Ndugu Mzee mkongea Alli kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa amewapongeza world vision kwa mradi huo wa maji. Baada ya kuijionea miundo mbinu ya maji na kujiridhisha kwa namna ilivyotekelezwa . Ndugu Mkongea Amesema mbio za mwenge wa uhuru zimeridhia kuufungua mradi huo.
Injinia wa maji Ndugu Egibert Mutarubukwa akieleza jambo mbele ya wakimbiza mwenge Kitaifa.
Mradi huu unahudumia takribani watu wapatao 2,155, zikiwemo shule na Zahanati. Kupatikana kwa maji kijijini hapa kumesaidia kupunguza magojwa ya mlipuko (Water born related diseases) hivyo kuimarisha afya za wananchi, kuongeza kipato na kukuza uchumi wa wananchi badala ya kupoteza muda mwingi kutafuta maji. Aidha, kuwepo kwa mradi huu kumesaidia Wanafunzi kupata muda wa kutosha katika kujifunza na kujisomea kwani watokapo mashuleni hutumia muda mchache wa kuchota maji.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa