• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MHE. JAFO ATOA MILLION 70 UJENZI WA BWENI KARATU SEKONDARI

Posted on: February 22nd, 2020

Na Tegemeo Kastus

Waziri wa Nchi Ofis ya Rais tawala za mikoa serikali za mitaa TAMISEMI ametembelea na kukagua miundo mbinu ya shule ya Sekondari Karatu. Mhe. Selemani Jafo ameambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha pamoja na Mkuu wa wilaya ya Karatu.

Mhe. Jafo ameambatana na mbunge wa jimbo la Karatu Mhe. William Qambaru pamoja na mbunge wa viti maalum wa wilaya ya karatu Mhe. Cecilia Pareso. Mhe.  Jafo amesema zaidi ya shilingi trillion 1.31 toka mwaka 2016 mpaka January 2020 zimetolewa kwa ajili ya mpango wa elimu bila malipo. Amesema uboreshaji wa miundo mbinu ya elimu umefanyika kwa shule za msingi shule za sekondari za kawaida, Mhe. Jafo amesema katika kuainisha shule kongwe zinazohitaji ukarabati walipata shule 89. Mpaka sasa shule 64 zimeshafanyiwa ukarabati nchi nzima, amesema namna shule hizo zilivyokuwa na sasa hivi ni vitu viwili tofauti.

Mhe. Jafo amesema wataalamu walisema shule ya sekondari ina nafuu lakini amesema hapana lazima sekondari Karatu ifanyiwe ukarabati. Amesema nataka iwe shule ya karatu iongoze kwa unadhifu na ubora wa majengo. Amesema uwekezaji katika elimu ndio unasababisha kiwango cha ufaulu kuongezeka sanaa. Amesema Karatu sekondari inakabiliwa pia na uhaba wa mabweni, amesema atatuma wataalamu kutoka Tamisemi ili wafanye tathimini ya kina ya majengo.

Mhe. Jafo ameahidi fedha za haraka za mwanzo kiasi cha million 70 kwa ajili ya ujenzi wa bweni moja wiki ijayo. Amesema bweni hilo litajengwa kwa force acoount ametoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya karatu kuanza kazi ya ujenzi wa bweni jumatano, amesema anataka kazi ya ujenzi wa bweni ikamilike ndani ya miezi miwili.

Mhe. Jafo amesema Karatu sekondari inafanya vizuri kitaaluma, lakini amesema wanauwezo mkubwa wa kufanya vizuri zaidi. Amesema anatamani sana kuhudhuria mahafali ya mwaka huu ya shule ya sekondari Karatu sekondari.  Amesema shauku yake ni kuona kila mtu Tanzania pindi matokeo ya kidato cha nne yanapotoka atamani  mtoto wake kwenda Karatu sekondari.

Mhe. Selemani Jafo katikati akiwa anatembelea eneo la shule ya sekondari Karatu.

Amewataka wanafunzi wa kidato cha tano na sita  kuazimia  kwamba hakuna zero, ametaka vijana kupambana kwa heshima ya Karatu sekondari. Ametaka vijana hao kuhakikisha Karatu sekondari kuwa katika shule 50 bora Tanzania katika ufaulu wa matokeo ya kidato cha sita.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa