• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MKAKATI MKALI WAJA KUWAKABILI WANASHERIA VIHIO

Posted on: February 7th, 2019

Maadhimisho ya siku ya sheria yamefanyika jana katika viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Karatu. Sherehe hizo zimeenda sambamba na kufungua mwaka mpya wa Mahakama na mgeni rasmi katika  maadhimisho hayo alikuwa ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo

 Maadhimisho hayo ya siku ya sheria yalikuwa na kauli mbiu inayosema; UTOAJI HAKI KWA WAKATI NA WAJIBU KWA MAHAKAMA NA WADAU. Mhe. Theresia Mahongo katika hotuba yake amewapongeza wadau sheria kwa kutumia siku hiyo kutoa elimu. Amesema elimu haina mwisho, wananchi wakipata elimu vizuri wanasheria wasio na taaluma  (Bush lawyers) hawana nafasi.

Mhe. Theresia amesema kushindwa kutolewa haki kwa wakati limekuwa ni tatizo kubwa, bado kuna watu kwenye Mahakama wanaojihusisha na vitendo vya rushwa. Mhe.Theresia amesema rushwa ni adui wa haki na uongozi wa awamu ya tano umekuwa ukikemea sana rushwa.

Mhe. Theresia amewaelekeza wanasheria kuja na mkakati wa kuwadhibiti Wanasheria wasio na taaluma (Bush lawyers). Wanasheria vihio wamekuwa wakiwaonea sana wananchi, Mhe Theresia amesisitza pia wananchi kupewa elimu ya namna ya kupewa dhamana. Amesema kumekuwa na mkanganyiko kwenye kutoa dhamana kuna wakati mdhaminiwa anatakiwa aje na Mwenyekiti wa kijiji maeneo ya kijijini na wakati mwingine Mwenyekiti wa kijiji anakataliwa na kutaka mtu anayehitaji dhamana kwenda  na Mtendaji wa Kata.

Mhe. Theresia amesema kuna mihimili mitatu ambayo ni Serikali, Mahakama, na Bunge. Amesema mihimili hii haingiliani katika kutekeleza majukumu yake, ameomba wananchi wenye kesi mahakamani au baraza la ardhi waendelee na kesi zao mpaka  zinapokwisha.

Mhe. Theresia amewaomba wananchi kutoa ushirikiano kwenye vyombo vya sheria ili wapate haki zao. Mahakamani kuna fomu za malalamiko ameomba wananchi wazitumie fomu hizo ili kero zao ziweze kutatuliwa.

Awali Hakimu Mkazi Mfawidhi Mhe. Kuppa amesema hakuna haki bila wajibu, kila mtu anapaswa kutoa haki. Kunyimwa haki ni uonevu mkubwa, nchi yenye misingi ya kikatiba na utawala wa sheria  Mahakama ndio chombo kinachotoa haki.

Mhe. Kuppa amesema Mahakama ya Wilaya ya Karatu imejiwekea utaratibu kwa Mahakama za Mwanzo uhai wa kesi  uwe ni miezi sita na Mahakama ya Wilaya uhai wa shauri lolote uwe ni miezi kumi na mbili na shauri la madai liwe miezi kumi. Amesema nakala za maamuzi au hukumu hutolewa  ndani ya siku ishirini na moja. Usipopata nakala kwa kipindi hicho unanza kufuatilia kwa Hakimu Mfawidhi wa kituo hicho.

Mhe. Kuppa amesema wadau wa Mahakama wanatakiwa kuwa na utamaduni wa kusuluhishana wao wenyewe kupitia katika ngazi ya familia na viongozi mbalimbali kwa mashauri ya kesi  ambayo hayana uzito mkubwa kwa mantiki ya adhabu zake kisheria.

Naye O.C. D wa Karatu S.P Musa Gumbo alisema kesi za madawa ya kulevya; nyara za serikali, au kesi za kuhujumu uchumi lazima vielelezo vipelekwe kwa Mkemia mkuu wa serikali. Baada ya hatua hizo lazima majalada yapelekwe kwa Mkurugenzi wa makosa ya jinai ndipo kibali cha kuendesha kesi kinapotolewa. S.P Musa Gumbo amesema ni matakwa ya kisheria kupeleka vielelezo kwa Mkemia mkuu wa serikali na Mkurugenzi wa makosa ya jinai bila kufanya hivyo upelelezi unakuwa haujakamilika na hii inasababisha kesi kuchukua muda mrefu.

 S.P Gumbo amesema kutoa haki kwa wakati kwa mashauri  kunategemeana na kuita mashahidi kwenye Mahakama kwa ajili ya kutoa ushahidi,  amesema huwa wanapata changamoto hasa pale wanapoita mashahidi wa mbali. S.P Gumbo amesema Mahakama huwa ni mkusanyiko wa Mahakama yenyewe, Waendesha Mashitaka na Mawakili. Afisa mmoja anapopata dhararura kati ya hawa Mwendesha mashitaka, Hakimu au Wakili kesi inaahirishwa na kupangiwa tarehe nyingine. Mashahidi hawa wengi wao wanatoka mbali na shahidi hulipwa pesa yake  baada ya kutoa ushahidi Mahakamani. Kutokana na changamoto kama hizo mashahidi huwa hawarudi Mahakamani kwa wakati pindi kesi inapoahirishwa na imekuwa ni kikwazo kikubwa  kuendesha kesi kwa wakati, kwenye makosa ya jinai

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa