• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MKUU WA WILAYA AFANYA ZIARA KATA YA MANG’OLA

Posted on: October 14th, 2021

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mhe. Abbas J. Kayanda  tarehe 13/10/2021 alizindua mradi wa Maji, Maktaba, Madarasa  na vyoo vya Wanafunzi shule ya Msingi Haydesh  iliyofadhiliwa na shirika la World vision ,pia alishukuru kwa niaba ya Serekali kwa namna World vision wamekuwa wakifadhili  miradi mingi ya maendeleo. Mkuu wa wilaya alielekeza fedha zote zitakazopatikana katika mradi huo wa maji zipelekwe Benki ili pindi matengenezo yanapohitajika iwe rahisi kufanyika na sio kusubiri mfadhili ,pia alielekeza Maktaba itumike vizuri ili kuongeza kiwango cha ufaulu.

Katika ziara hiyo Mkuu wa Wilaya alipata nafasi ya kufanya mkutano wa hadhara Mang’ola Barazani lengo ni kusikiliza kero za wananchi . Wananchi walitoa kero mbalimbali za Maji, Umeme,na Upimaji wa Ardhi.

Kero ya Maji, Maji kutokufika Shule ya Sekondari Anagamazo, Kaimu Meneja wa RUWASA Ndg Ayoub Feswal alitoa ufafanuzi kuwa kwa kushirikiana na World Vision na Wakala wa maji Vijijini (RUWASA) kwa mipango waliojiwekea watahakikisha maji yanafika shuleni hapo.

Umeme, baadhi ya vijiji kutokufikiwa na umeme wa REA Mkuu wa wa Wilaya aliwaambia kwa sasa mkandarasi yupo maeneo mengine na kuwataka  Wananchi wawe na subira watafikiwa na Umeme.

Upimaji wa ardhi, Mji wa Mang’ola unakuwa kwa kasi wananchi wanahitaji kupimiwa maeneo yao ili kuyapa thamani, Mkuu wa Wilaya aliwambia wananchi wataaalam wa aridhi walishafanya tathimini ya upimaji na kuwataka Wananchi kujitokeza kuchangia fedha kwenye Akaunti iliyofunguliwa ili wapimiwe kwa pamoja. Pia  Mkuu wa Wilaya aliwaambia Wananchi Serikali imeleta fedha 1.6bil kwa ajili ya ujenzi wa vyumba 58 vya madarasa kwa Shule za Sekondari.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha hizo kwa wananchi wa Karatu na kuahidi kusimamia matumizi ya fedha hizo kwenye ujenzi wa madarasa.

Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya Abbas J. Kayanda akikakagua Mradi wa Maji katika Shule ya Msingi Haydesh

Mkuu wa Wilaya Mhe. Abbas J. Kayanda akikagua Mktaba ya kisasa Shule ya Msingi Hydesh


Mkuu wa Wilaya Mhe Abbas J. Kayanda akizindua madarasa Mawili ya Kisasa yaliyofadhiliwa na World

Vision

Mkuu wa Wilaya Mhe Abbas J Kayanda akizungumza nan a wananchi wa Mang’ola Barazani katika uwanja wa mikutano.

Mhe. Jacob P. Welwel Diwani Kata ya Mang’ola Barazani akifafanua jambo katika Mkutano wa mkuu wa Wilaya


Wananchi wa rika mbalimbali waliojitokeza katika mkutano wa Mkuu wa Wilaya


Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa