Mwenge wa uhuru umeweka jiwe la msingi katika kituo cha afya Endabash, kituo hicho kimejengwa kupitia fedha million mia nne ilizopewa Halmashauri kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa miundo mbinu. Fedha hizo zimetolewa kupitia force account na umeshirikisha wananchi na wadau mbalimbali.
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Ndugu Mzee Mkongea, amesema kuna baadhi ya milango haifunguki vizuri amemuelekeza injinia kurekebisha milango hiyo. Kwenye bafu la chumba kuogesha maiti ni vizuri ikawekewa shata. Mfumo wa maji taka na safi ni vizuri ukatenganishwa kwenye jengo hilo. Ameomba mradi ukamilke kwa wakati na wameridhia kuuwekea jiwe la msingi mradi wa afya kituo cha Endabash.
Miradi mipya iliyojengwa ni wodi ya watoto, ambayo kiasi cha fedha kilichotumika kwa fedha za ufundi tu ni shilingi 11998,500, nyumba ya mtumishi ambayo kiasi cha shilingi 6,232,000 na jengo la kuhifadhi maiti ambayo kiasi cha 5,692,375 na wodi ya wazazi ambayo kiasi cha 12,896,250. Fedha hizo ukijumuisha na maksio ya gharama za vifaa vya ufundi unapata jumla ya shilingi 346,822,862.
Fedha zilizobakia katika ujenzi huo ambazo ni shilingi 53,177,137 zinatarajia kufanya ukarabati wa jengo la wagonjwa wa nje. Fedha hizo zitatumika kutengeneza njia ya kupita wagonjwa na chumba cha upasuaji.
Kijiji cha Endabash kimechangia nguvu kazi kwa kukusanya mawe kushusha kokoto tripu 48 na kusawazisha maeneo ya ujenzi. Kijiji pia kimechimba msingi wa majengo yote na kuchimba mashimo ya kuhifadhi maji taka, kuchimba mtaro, kununu mabomba ya majina kuyalaza ili kufikisha maji kwenye ujenzi eneo la kituo cha afya mita 300 pamoja na kununua tanki la kuhifadhi maji wakati wa ujenzi. Nguvu hiyo waliochangia ni sawa na kiasi cha shilingi 19,800,0000
Halmashauri imechangia baadhi ya shughuli ikiwemo kutoa lori lillilotumika kusafirshia mchanga. Kutoa wataalamu kwa ajili ya usimamizi wa mradi huo ambao ni sawa na shilling 8,800,000 na kufanya thamani ya jumla ya mradi kufika shilingi 428,600,000.
Wakimbiza mwenge kitaifa wakikagua jengo la kuhifdhi maiti, kituo cha afya Endabash.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa