• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

MRADI WA UJENZI WA SOKO

Posted on: June 16th, 2021

Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Luteni Josephine Paul Mwamabashi ameweka jiwe la msingi katika mradi wa soko kuu la Karatu. Luteni Mwambashi ameelekeza watendaji wa serikali kufanya mikutano na wananchi kuwaeleza hatua zilizofikiwa na mradi na mipango ya ukamilishaji wa ujenzi wa soko hilo.

 kukamilika kwa mradi huu wa soko kutawawezesha Wakulima, Wafugaji na Wavuvi wa Karatu kupata sehemu ya kupeleka mazao yao kuuza kutokana na changamoto ya kutokuwa na soko la kuuzia mazao ambayo imekuwa ikiwakabili Wakulima, Wafugaji na wavuvi katika Wilaya ya Karatu ambayo asilimia 85 ya wakazi wake kujishughulisha na Kilimo, Ufugaji na Uvuvi. Soko hili litaongeza mnyoyoro wa thamani ya mazao kwa upande wa masoko. Mazao Makuu yanayotarajiwa kupelekwa sokoni ambapo kuna vizimba 2020 na vibanda 27 ni pamoja na Mahindi, Maharage, vitunguu, pia kuna mazao ya mifugo kama vile nyama, mayai na samaki. Pia wateja wanao nunua mazao mbalimbali watakuwa na sehemu moja ya uhakika ya kupata mahitaji yao kwa wakati mmoja. Soko hili vile vile ni chanzo cha mapato ya ndani ya Halmashauri kupitia kodi ya pango la vizimba na vibanda.

Ujenzi ulianza mwezi Aprili 2018, hadi sasa mradi huu umegharimu jumla ya Tsh 580,447,399.00 kwa mchanganuo ufuatao; Malipo ya mafundi ni Tsh 85,606,070.00 , Ununuzi wa vifaa vya ujenzi ni Tsh 485,883,329.00 na Mafuta ni Tsh 8,958,000.00

Mambo yaliyofanyika katika ujenzi wa soko hilo ni pamoja na ujenzi wa nguzo mlalo (beams) na nguzo wima (column); Upigaji wa makenchi yote na kupiga bati, Usukaji wa nondo kwenye nguzo mlalo (beams), nguzo wima (column) na slebu pamoja na umwagaji zege kwenye ghorofa,

Ujenzi wa mfereji wa kukusanya maji ya mvua, Jumla ya vizimba 202 vimejengwa, vimemiminwa zege la slebu, kuwekewa milango, kupigwa ripu na kupakwa rangi jumla ya maduka 27 yamejengwa na kupigwa ripu, Usukaji wa mfumo wa umeme kwa soko zima unaendelea bado kufunga mita ya umeme. Aidha kwa sasa kazi ya kuziba eneo la juu la soko kwa kutumia bati zinazoruhusu mwanga imekamilika.

matukio katika picha wakat kiongozi wa mbio za mwenge alipotembelea na kuweka jiwe la msingi mradi wa soko kuu karatu

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa