Mwenge wa uhuru umezindua nyumba za walimu pamoja na bweni la wasichana katika shule ya Baray khusumay. Shule hiyo ni moja ya shule 35 za sekondari zilizopo katika wilaya ya Karatu zenye wanafunzi 12683 na walimu 594.
Kiongozi wa mwenge kitaifa Ndugu Mzee Mkongea Alli amesema nyumba za walimu sehemu ya kuoshea vyombo haina kichujio. Amesema kuna baadhi ya milango haifunguki mpaka mwisho, pia amesema ni vyema wakaweka taga za kusaidia kuvuna maji. Ndugu Mkongea amempongeza Mhandisi kwa ubunifu mkubwa alioufanya katika ujenzi wa bweni pamoja na nyumba mbili za walimu two in one.Amesema Mhandisi ameweka kichomeo taka lakini kwenye bweni ameweka kabati za chuma za kuhifadhi vifaa kwa ajili ya wanafunzi.
kiongozi wa mbio za mwenge akikagua mfumo wa maji katika bweni la wasichana la Baray Khusumay
Ujenzi wa majengo matatu (Nyumba mbili za walimu na Bweni la wasichana umegharimu jumla ya Shilingi 298,562,654.50, ambazo michango ya Wananchi ina thamani ya Shilingi 27,142,059.50 na TASAF imechangia kiasi cha Shilingi 271,420,595.
Kukamilika kwa Miradi hii ya Nyumba mbili za Walimu na Bweni la wasichana kumewezesha shule kukidhi vigezo vya kusajiliwa na pia kuwezesha kuongeza idadi ya Walimu katika Shule hii na kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na hatimaye kupandisha ubora wa elimu na kiwango cha ufaulu cha wanafunzi.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa