Kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Ndugu Mzee Mkongea Alli amezindua barabara ya NBC- KUDU yenye umbali wa 0.6 km kwa kiwango cha lami. Mradi huo unasimamiwa na wakala wa barabara vijijini na mjini TARURA.
Ndugu Mzee Mkongea amesema mistari ya alama za barabarani zimefutika, lakini kwenye mifereji kuna alama za nyufa. Amesema kuna baadhi ya maeneo barabara, ina makorongo Ndugu Mkongea ametoa maelekezo, barabara hiyo kufanyiwa marekebisho ndani ya wiki mbili kwa sababu mkandarasi aliyejenga barabara bado yupo katika kipindi cha matazamio. Ndugu Mkongea amesema ameridhishwa na vipimo vya maabara, hivyo mbio zimeridhia kuuzindua mradi huo wa barabara.
Mkimbiza Mwenge akichukua vipimo vya urefu wa barababra.
Ujenzi wa mradi huo umefanywa na mkandarasi Mkandarasi M/S Jonenac Construction Ltd. Mradi ulianza tarehe 08/03/2018 na kukamilika tarehe 27/09/2018. Kazi zilizofanyika ni kuchimba na kujenga mifereji yenye jumla ya urefu wa mita 400 kwa ajili ya kupitisha maji ya mvua, kuweka lami nyepesi mita 600 na kujenga Makalvati mawili (2).
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa