NA TEGEMEO KASTUS
Kikosi kazi maalumu kitakachohusisha maaskari wa hifadhi ya ziwa Manyara (TANAPA) na Mamlaka ya Ngorongoro wakisaidiana maaskari wanyamapori wa Halmashauri ya Karatu watafanya kazi ya kusaka fisi anayekula watu katika kata ya Endamarariek.
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Basodawish. Amesema licha ya hatua zitakazochukuliwa na serikali za kumsaka fisi huyo ambaye anajitokeza katika mazingira ya kutatanisha na hali ng'ombe wala mbuzi anakula watoto wadogo. Mh. Kayanda ametangaza siku mbili za maombi kila kijiji katika kata hiyo ili kumuomba mwenyezi Mungu kuepusha janga hilo na siku ya tatu ya maombi yatafanyika Makao Makuu ya kata na yataongozwa na viongozi wa dini wa kata pamoja na Wilaya.
Mh. Kayanda amesema katika kijiji cha Basodawish yametokea matukio sita na matukio mawili yamegharimu uhai wa watu. Kijiji cha Shangt yametokea mashambulizi mawili kati ya hayo matukio watoto wawili walijeruhiwa na watoto wawili walifariki dunia. Katika kijiji cha Endamarariek limetokea tukio la mtoto kujeruhiwa na tukio jingine kugharimu uhai wa mtoto. Katika kijiji cha Gidbaso liltokea tukio moja lakini hakuna mtoto aliyejeruhiwa. Amesema katika matukio kumi jumla yaliyotokea tangu mwaka 2019 kati ya hayo matukio matatu yametokea mwaka 2020 ambayo mawili ndio yamesababisha vifo na moja mtoto kujeruhiwa.
Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi katika mkutano wa hadhara kijiji cha Basodawish.
Wakati akifungua kikao hicho Mwenyekiti wa kijiji cha Basodawish Ndg. Meta Petro Bare amesema katika siku tatu fisi amekuwa hatare sana kwa uhai wa watu. Amesema kwa mtirirko wa matukio inaonekana ni fisi mmoja tu anayesumbua eneo zima la kata ya Endamarariek. Amesema tukio la juzi kuna mtoto aliyeng’atwa na fisi na kuna binti ambaye pia aling’atwa na fisi. Amesema hali ya binti inaendelea vizuri na ameruhusiwa kutoka hospital na mtoto aliyevamiwa na fisi amepelekwa katika kituo cha afya cha Fame na alikuwa katika hatua za kufanyiwa upasuaji.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa