• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

SERIKALI YATOA FEDHA KUKARABATI ZAHANATI JOBAJ

Posted on: February 17th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Wananchi mnapaswa kujivunia uboreshaji wa huduma za afya kwa wananchi unaofanywa na serikali. Zahanati ya Jobaj  ni moja ya zahanati tatu wilayani Karatu zilizopata million hamsini kwa ajili ya ukarabati wa zahanati.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokagua jengo la nyumba ya mganga  lilojengwa kwa nguvu ya wananchi. Amewapongeza wananchi hao kwa moyo wa kizalendo wa kuboresha miundo mbinu ya afya. Amesema serikali imetoa fedha kwa ajili ya kukarabati zahanati ya Jobaj zahanati ya Mang’ola juu, na zahanati ya kijiji cha huduma ambazo kwa pamoja zimepata kiasi cha million 150. Amesema zahanati hizo zikishamaliza kukarabatiwa majengo, huduma za afya zitakuwa za kisasa.

Katika ziara hiyo mkuu wa wilaya alikagua hali ya upatikanaji wa dawa na kufanya mkutano wa hadhara. Amesema serikali ya awamu ya tano inyoongozwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli imeboresha huduma za afya kwa kiwango kikubwa. Amesema kuna makundi maalum ambayo yanapata huduma za afya bure kama watoto chini ya miaka 5 kinamama wajawazito na wazee ambayo kwa vituo vya afya vya binafsi wanalazimika kutoa fedha.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akikagua zahanati ya Jobaj.

Amesema zahanati ya Jobaj ina uwezo wa kuhudumia wakinamama wajawazito kati ya 12 mpaka kinama 13. Amesema wananchi wakijiunga na mfuko wa bima ya afya utasaidia kuongeza upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo. Hivyo ametoa rai kwa wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ili iweze kujengea uwezo zahanati hiyo kupata dawa nyingi ambazo zitasaidia kuimarisha hali ya upatikanaji wa dawa.

Katika hatua nyingine Mh. Kayanda amewaomba wananchi kupeleka watoto waliochaguliwa kidato cha kwanza kwenda  shule. Amesema hakuna urithi mkubwa utakaomuachia mtoto kama elimu. Ameongeza kusema mtoto akisoma inamsaidia kujenga misingi bora ya kujitegemea, ambayo ni tofauti na mtoto aliyenyimwa kwenda shule. Mtoto aende shule hata kama hana sare ili mzazi utafute sare wakati mtoto akiendelea kusoma.

Katika mkutano huo wa hadhara Mh. Kayanda ametoa maelekezo mahususi kwa wazazi wa kijiji cha Jobaj kuhakikisha wanachangia chakula kama walivyokubaliana katika mkutano wa kijiji. Ameelekeza mwisho wa kuchangia chakula uwe mwezi wa pili mwishoni, na  ameelekeza eneo la shamba la shule ya msingi Jobaj, ambalo serikali ya kijiji  ikishirikiana na wazazi iliazimia kulilima mwezi wa tisa mwaka huu wahakikishe wanaanza  kulima kwa kuzalisha mahindi ili kusaidia upatikanaji wa chakula kwa wanafunzi wa shule ya msingi Jobaj.

Amesema malengo yaliowekwa na serikali ya kijiji ya kutenga sehemu ya shamba la shule, ni makakati mzuri wazazi wanatakiwa kusimamia ili kuhakikisha uzalishaji wa chakula cha wanafunzi unafanikiwa.

Wananchi wakichangia  katika mkutano huo ndugu Emmanuel Mgana amesema swala la afya halina mbadala. Amesema ni vyema kukata bima ya afya iliyoboreshwa iwe sheria badala ya kuwa swala la hiari kwa sababu itasaidia  zahanati ya jobaj kupata dawa za kutosha.

Mh.  Abbbas Kayanda akiwa katika mkutano wa hadhara katika kijiji cha Jobaj.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa