• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

SIMPA, AOMBA MPANGO MADHUBUTI KUHIFADHI VYANZO VYA MAJI

Posted on: November 7th, 2019

Kikao cha baraza la madiwani  Halmashauri ya wilaya ya Karatu cha robo ya kwanza ya Mwaka wa fedha 2019-2020 kimekaa na kujadili taarifa za maendeleo za kata. Kikao hicho kimeongozwa na Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Emmanuel Gege.

Mhe. Elias Simpa diwani wa kata ya Mbulumbulu amesema katika taarifa yake kwamba wananchi wa kata ya Mbulumbulu wanapata changamoto ya kutopata  huduma ya maji safi kipindi cha kiangazi kwa sababu maji wanayotegemea kwa matumizi ya manyumbani yanatoka chanzo cha hifadhi ya Ngorongo.  Maji huwa yamechafuka kwa sababu wananchi wa maaeneo mengine hunywesha mifugo katika vyanzo vya maji  hivyo kuathiri wananchi wa ukanda wa chini wanaotegemea maji ya matumizi ya manyumbani kutoka  katika hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro.

Mhe. Elias Simpa amesema kwa upande wa kata ya Mbulumbulu wao wameelimisha wanaanchi umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji na wameelewa. Ameomba baraza la madiwani la  Halmashauri ya wilaya Karatu kulipa msukumo swala hilo ili wananchi wa maeneo mengine wanaozunguka chanzo hicho waone umuhimu wa kuhifadhi vyanzo vya maji. Adha wanayopata wananchi wa kata ya Mbulumbu ni pamoja na wakati mwingine kulazimika kutumia maji ya rangirangi kutokana na mifugo kutifua na kuvuruga vyanzo vya maji.

Watendaji wa Halmashauri ya Karatu wakiwa katika kikao cha baraza la madiwani.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe. Simon Bajuta amesema tayari wameshakaa vikao vya ujirani mwema kati yao na mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro madiwani wa Halmashauri ya Ngorongoro na Monduli kujadili swala hilo kwa kina ili kuja na ufumbuzi wa pamoja wa changamoto hiyo. Amesema wamekubaliana katika kikao hicho kwamba wananchi wasinyeshwe mifugo katika vyanzo vya maji.

Afisa wanyamapori wa wilaya ya Karatu Bi, Donata Kimario amesema wilaya ya Karatu imepakana na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro. Amesema  msitu wa nyanda za juu kaskazini umehifadhiwa kwa ajili ya wanyama na vyanzo vya maji. Eneo hilo linalindwa na mamlaka ya hifadhi ya ngorongoro, ameomba mamlka hiyo kuongeza ulinzi katika vyanzo vya maji ili wananchi wasitumie kunywesha mifugo katika maeneo ya vyanzo vya maji ili kuepeuka uchafuzi wa maji yanayotegemewa kwaajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani

Mwenyekiti wa Halmashauri Mhe.Emmanuel Gege amesema maji ya Manyumbani wanayotumia wananchi wa Wilaya ya Karatu, vyanzo vyake vinatoka hifadhi ya mamlaka ya Ngorongoro. Amesema wao wanaamini katika mazungumzo ndio maana wanakaa vikao vya ujirani mwema ili kuja na ufumbuzi wa kutatua swala hilo kwa pamoja.

Madiwani wakiwa katika kikao cha robo ya kwanza cha baraza.

Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa