• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

SIPENDI KUONA MTU ANAONEWA !!!

Posted on: August 6th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Halmashauri ya wilaya ya Karatu imefanikiwa kukusanya 93% ya mapato ya kodi ya ndani kwa mwaka wa fedha uliopita. Kiwango hicho hakiwahi kufikiwa tangu Halmashauri ya wilaya ya karatu ilipoanzishwa.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akizungumza na wafanyakazi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Amesema Halmashauri imefika hapo kwa sababu ya team work. Mkurugenzi hawezi kufanya hizi kazi peke yake lazima apate ushirikiano na kutoka kwa wakuu wa idara na watumishi wengine wa ngazi za chini. Mh. Kayanda amesema kwenye maswala ya lishe na ICHF Halmashauri imeshika nafasi ya pili kwa ngazi ya mkoa. Amesema ufaulu wa elimu ya msingi umetoka wastani wa 65% mpaka kufikia 82. 

Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda akizungumza na watumishi wa Halmashauri ya Karatu

Mh. Kayanda amesema watumishi wanatakiwa wawe na maadili na wanatakiwa wayaishi Maadili ya utumishi wa umma  nje na ndani ya ofisi. Lazima watumishi wavae mavazi yanayoendana na maadili ya utumishi wa umma, amesema mtumishi anawajibika kutunza mali za serikali. 

Mh. Abbas Kayanda akiwa anazungumza  na watumishi wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu.

 Mh. Kayanda amesema Migogoro ya ardhi iliyodumu  muda mrefu lazima imalizwe,  amesema hapendi kuona wananchi wakisumbuliwa kupata haki zao. Amesema lazima watumishi wote wawe kitu kimoja, ikitokea mtu mmoja anavuta kurudi nyuma atasababisha kurudi nyuma watu wote ikitokea mtu anavuta mbele atasababisha watu wote  kwenda mbele. Amesema ushirikiano ni jambo la muhimu sana katika utendaji  wa kazi, amesema ni vyema watu kufanya kazi kwa kuzingatia miongozo ya kazi.

Mh. Kayanda amesema kila mtumishi ana nafasi yake amesema hapendi kuona mtu anaonewa kwa sababu ya udogo wake katika kazi  amesema mtu kama anaadhibiwa basi aadhibiwe kwa makosa aliyoyafanya. Amesema kama mtu anapongezwa apongezwe kwa sabababu ya ufanisi wake katika kazi. Amesema ni vizuri watumishi kuheshimu mipaka ya kazi na kuheshimu mipaka ya kazi ya watumishi wengine.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa