• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

SUPERVISION; ZILETEE MATOKEO CHANYA VITUO VYA AFYA

Posted on: April 6th, 2021

Watumishi wa idara ya afya waanze utaratibu wa kubandika kwenye vituo vya afya dawa zinazopatikana. Ili kumsaidia mwananchi anapoenda zahanati au ngazi ya kituo cha afya kujua ni dawa za aina gani zinapatikana, kuainisha aina za dawa itasaidia kuondoa malalamiko kwa wananchi kwamba vituo vya kutolea huduma za afya havina dawa.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh.Abbas Kayanda wakati alipotembelea zahanati ya Dofa kujionea hali ya utoaji wa huduma na upatikanaji wa dawa. Amesema wananchi wanapaswa kufahamu katika ngazi ya zahanati dawa za aina gani zainapatikana, ngazi ya kituo cha afya dawa za aina gani zinapatikana ili kujenga uelewa wa pamoja.

Mh. Abbas Kayanda (kushoto) akikagua hali ya upatikanaji wa dawa katika kituo cha afya Dofa

Mh. Kayanda amewalekeza watumishi wa idara ya afya kuhakikisha huduma katika vituo vya zinaboreshwa na kuzingatia  kuweka mazingira rafiki ya kutolea huduma. Mh. Kayanda amesema  chumba cha uzazi, chumba cha sindano chumba cha kusafisha majeraha ya vidonda lazima viwe na faragha inayomuwezesha mgonjwa kusitirika wakati akipata huduma. Badala ya utaratibu wa sasa ambao vyumba hivyo havioneshi namna ya kumsitiri ugonjwa wakati akipewa huduma.

Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda amewaelekeza watendaji wa vijiji na kata kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa bima ya afya iliyoboreshwa ili kuongezea kituo uwezo wa kupata dawa. Amesema idadi ya wakinama wanaojifungulia hospitali ni ndogo jambo hilo linatokana na mwamuko kuwa mdogo kwa wananchi. Lazima jitihada za kuelimisha wananchi kujifunglia hospitali ziongezwe ili wananchi wahamasike kupata huduma katika vituo vya afya.

Mh. Kayanda amesema hata supervision zinazofanyika na wataalam wa afya lazima zilete matokeo chanya. Taarifa za ukaguzi ziwe ndio sehemu ya kujitathimini utendaji wa watumishi vituo vya afya ili kuja na njia za kuboresha huduma za afya.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa