• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

TAKUKURU KARATU WAOKOA MILLION 21 ZA MSTAAFU

Posted on: September 22nd, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa wilayani Karatu imeokoa kiasi cha million 21 na laki moja kwa Mwalimu Mstaafu. Fedha hizo zilikuwa zimeporwa na kampuni ya Robby credit Company limited inayomilikiwa na Emmanuel Bonifasi tangu February Mwaka 2019.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amesema Mzee Pilonga Vicent alienda kukopa fedha kwenye taasisi ya kifedha ya Robby credit kiasi cha million 3 kwa makubaliano ya kurudisha kiasi cha fedha hizo na riba ya  30%. Amesema baada ya kuingia kwa fedha yake ya kusataafu million 25 fedha zote zilichukuliwa na taasisi ya Robby credit.

Mh. Kayanda amesema vyombo vya habari vimemsaidia kujenga elimu ya uelewa  Mzee Pilonga  juu ya namna taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa inaweza kumsaidia. Amesema Takukuru walichunguza kwa undani jambo la Mzee Pilonga na kugundua kwamba taasisi ya Robby credit ilichukua kadi ya bank na pamoja na numba yake ya siri. Amesema hiyo ilichangia fedha za Mzee Pilonga kuchukuliwa na taasisi ya Robby credit.

Mh . Kayanda amesema watendaji wa Takukuru walilisimamia jambo hilo na viongozi wa Robby credit walikiri makosa waliyoyafanya na kurudisha fedha hizo. Mh. Kayanda ametoa wito kwa wananchi ambao wamedhulumiwa katika taasisi za kifedha na wanaushahidi wawasilishe malalamiko katika taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa. Amesema hata wananchi wanaoenda katika taasisi za umma kupata huduma, kama kuna vitendo vyovyote vinavyoashiria rushwa wasisite kutoa taarifa Takukuru ili kudhibiti  vitendo vinavyoharibu taswira ya utendaji kazi.

Awali katika taarifa yake Naibu wa takukuru Arusha Sabasi Salehe amesema matatizo hayo yamezidi kuongezeka mkoani Arusha. Amesema wameanza kurejesha fedha nyingi, amesema hushughulikia watuhumiwa kwa njia mbili kwanza kwa kuchunguza kwa kina na kujiridhisha kama Mtuhumiwa aliyefanya alifanya pasipokujua, kama ni kweli akirejesha fedha alizochukua anasamehewa na kuonywa. Amesema kuna watuhumiwa ambao wanavunja sheria ya Takukuru No1 ya mwaka 2017  hivyo sheria inachukuliwa dhidi yao.

Mh. Abbas Kayanda (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na Mzee Pilonga pamoja na maafisa wa Takukuru

Kamanda wa Takukuru wilaya ya Karatu Bi. Atuganile Stephen amesema wananchi wenye mikopo umiza watoe taarifa ofisini ikiwa ni pamoja na watu wenye taarifa za vitendo vya rushwa.  Amesema jukumu la kupambana na rushwa ni letu sote .

Naye mtaafu aliyerejeshewa fedha zake Mzee Pilonga amesema anajisikia amani yake imerejea kwa sababu alikuwa anawaza analeaje familia kutokana na unyang’anyi aliofanyiwa. Amesema lakini kutokana na juhudi za serikali kupitia Takukuru fedha zake zimepatikana, Mzee Pilonga ameishukuru  sana  serikali kwa msaada aliopata.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa