• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

TUJIFUNZE KUHUSU AFYA

Posted on: June 7th, 2019

Kasi ya magonjwa yanayoambukizwa kwa njia ya ngono isiyo salama imeongezeka duniani. Utafiti uliofanywa na shirika la afya WHO na baadae taarifa yake kutolewa na kituo cha televisheni cha CNN umesema karibu kila watu 25 mtu mmoja anadalili za magonjwa yanayosababisha na ngono isiyo salama.

Dkt. Mellanie Taylor aliyeongoza utafiti huo uliotolewa Alhamisi anasema watu wamekuwa wanajihusisha na mahusiano ya ngono hatarishi kiafya. Tabia zinazo sababisha magonjwa ya ngono (sexual trasnsmited disease Infection) STIs ambayo pia hufahamika kama STD’s. Dkt. Mellanie anasema magonjwa kama Kaswende Gonorea upungufu wa kinga mwilini ni miongoni mwa magonjwa ambayo husababishwa na kufanya ngono isiyo salama.

Dkt. Vicent Gyunda ni daktari kiongozi katika kituo cha afya Karatu. Dkt. Vicent anasema ni kweli ngono isiyo salama inasababisha magonjwa ya zinaa. Anasema kwa takwimu za Mwaka huu January mpaka March yaliripoitiwa matukio 1879 ndani ya wilaya ya Karatu kati ya hayo matukio 219 yaliripotiwa kituo cha afya Karatu.



Dkt  Vicent Gyunda

Dkt. Vicent anasema magonjwa hayo yamegawanyika kwa makundi; yapo magonjwa yanatokana na Genital discharge syndrome, ambayo ni mlundikano wa magonjwa kama Gonorea. Kuna kundi la magonjwa yanayotokana na Genital ulcer diseases, ambayo inakuwa kama mchubuko au kidonda kisichokuwa na maumivu yeyote sehemu za siri. Hii hujitokeza kwa mtu mwenye magonjwa kama kaswende. Kuna magonjwa yanahusu jinsia ya kike katika kundi hili kuna Pervic inflammatory disease. Hii huhusisha viungo vyenye mahusiano na tendo la ngono ambayo husababisha viungo vya uzazi; kama nyumba ya uzazi, shingo ya kizazi , nyonga kupata maambukizi haya yanayofuata mfumo huu wa viungo vya uzazi  ambavyo huaathirika kwa pamoja na hutokea hasa kwa wanawake. Dalili zake ni mauvimu chini ya tumbo, ambayo pia husababisha badiliko asili la umbo kama kuwa na wekundu na kuondoa muonekano wa kawaida.

Dkt. Vicent anasema visababishi vya magonjwa haya ni mazingira hatarishi. Dkt vicent anasema kuwa na mahusiano na mtu zaidi ya mmoja ni chanzo kwa sababu cha watu kufanya ngono hatarishi ambayo muathirika anapata kwa kushindwa kutumia kinga. Dkt vicent anasema hali ya umasikini husababisha baadhi ya watu kujiingiza katika ngono hatarishi kutokana na uduni wa kipato.

Dkt. Vicent anasema upo pia uwezekano wa mama mjamzito kumuambukiza mtoto mchanga haya magonjwa wakati wa kujifungua, kutokana na michimbuko au msuguano wakati wa kujifungua. Dkt vicent anasema kuna swala la mila potofu, ambazo husababisha kuzidi kuenea kwa  magonjwa yatokanayo na ngono zembe. Imani za kuridhishana wajane au kufanya ngono na mtu wa rika flani ili ufanikiwe kupata fedha.

Dkt Vicent anasema kuna visababishi ambavyo ni kama wakala wa kusambaza maradhi, mathalani virusi ambavyo huleta magonjwa kama Upungufu wa kinga mwilini. Kuna bacteria  ambao husambaza magonjwa  yanayotokana na ngono zembe. Lakini kuna protozoa ambao husambaza magonjwa yanayotokana na ngono zembe.

Dkt. Vicent anasema namna kuepuka madhara ya magonjwa yanayosababishwa na ngono zembe ni kuacha kufanya ngono zembe kwa kujizuia tamaa za mwili. Dkt. Vicent anasema  tunashauri kama mtu hawezi kujizuia tama za mwili, kutumia mpira ambao utamkinga na magonjwa hatari yanayotokana na ngono zembe. Dkt vicent anasema njia nyingine sahihi ni kuwahi kupata tiba mtu aliyeathirika ambayo husaidia kupunguza maumbukizi mapya. Dkt vicent anasema wao kama idara ya afya hujikita kutoa elimu kwa wananchi  kupitia kliniki za mkoba.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa