• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

TUZITANGAZE FURSA ZA UWEKEZAJI KARATU

Posted on: April 23rd, 2021

Na Tegemeo Kastus

Sekta binafsi ndio waajiri wakubwa  na walipaji wakubwa wa kodi ya serikali, sekta binafsi ndio wachangiaji wakubwa wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali. Kazi ya serikali ni kuimarisha ulinzi na usalama ili kuwezesha taasisi binafsi ziwe na mazingira wezeshi kwa wawekezaji kufanya kazi vizuri. Lazima tuwe na eneo kwa ajili ya uwekezaji kwa ajili ya kuwavutia kufanya shughuli za biashara.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipokuwa akizungumza katika kikao cha baraza la biashara la wilaya ya Karatu kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri. Amesema lazima baraza la biashara liwe na one stop centre sehemu ambayo muwekezaji atapata taarifa mbalimbali za fursa za uwekezaji  zinazopatikana katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu.

Wajumbe wa baraza la biashara la wilaya ya Karatu wakiwa katika kikao

Mh. Kayanda amesema kuna fursa ya kupeleka mazao ya vitunguu nchini Qatari lakini wananchi hawafahamu kama kuna fursa hiyo. Kuna wawekezaji wa kutoka nchini Kenya wanataka kujenga kiwanda cha kuchakata mbaazi, kama tunahitaji kuleta mabadiliko ya kiuchumi inabidi tuanze kutengeneza mazingira wezeshi ya uwekekzaji.

Mh. Kayanda amesema ni jukumu la Halmashauri kutangaza fursa zinazopatikana ili kujenga uelewa mkubwa kwa wananchi, ameongeza kusema kama hatutaweza kuwekeza na uwekezaji utaendelea kuwa duni. Ametoa mwelekeo kwa baraza la biashara kuja na taarifa za fursa za uwekezaji zinazopatikana katika Halmashauri ya wilaya ya Karatu. Ametumia nafasi hiyo kulitakia heri baraza linalomaliza muda wake wa uongozi baada kufanya kazi kwa kipindi cha miaka minne. Amesema baraza hilo limefanya kazi nzuri na nijukumu la wajumbe wapya wa baraza la biashara kubeba na kuhuisha jitihada zilizofanywa.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu Mh. John Lucian akizungumza katika kikao hicho amesema Halmashauri itaweka mfumo mzuri wa mawasiliano na ushirikiano mkubwa kwa baraza la biashara. Ikiwa ni pamoja na kujikita katika kutoa elimu kwa wananchi na umma juu ya fursa za uwekezaji zinazopatikana. Ikiwa ni sambamba na Halmashauri kutenga eneo maalumu kwa ajili ya wawekezaji  kujenga viwanda.

Amesema Halmashauri inakusanya ushuru katika sekta ya mifugo sekta ya kilimo na sekta ya biashara ili kupata fedha zinazosaidia kutekeleza miradi ya maendeleo. Mh. Lucian amesema Halmashauri itaweka sera nzuri, na mazingira rafiki kwa sekta zote ili muwekezaji anufaike na uwekezaji atakaoufanya na aweze kutoa ushuru kwa Halmashauri.

Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wajumbe wa baraza la biashara la wilaya ya Karatu.

Ndg. Charles Goranga Mwenyekiti wa baraza la biashara linalomaliza muda wake wilaya ya Karatu amesema vikao vya baraza la biashara vimekuwa vikisuasua kufanyika kutokana na ushirikiano duni uliokuwepo awali.

Amesema ni wakati sasa kwa baraza la biashara kufanya kazi kwa pamoja na wadau wengine ili kuendana na kasi ya mahitaji ya watu.

Akichangia katika kikao cha baraza la biashara Mkuu wa kituo cha polisi Karatu ndg. Henry Mwansansu amesema kuna malalamiko makubwa ya kukosekana kwa soko la mahindi. Hivyo kuongeza vitendo vya udanganyifu kwa wakulima katika biashara ya mazao ya chakula, amesema ni vyema baraza la biashara likasaidia kuwalekeza wakulima njia bora za kupata wateja wa zao la mahindi. Amesema kesi za utapeli wa uuzaji wa zao la mahindi zimeongezeka kutokana na wakulima kutokuwa na taarifa sahihi za bei ya soko na sehemu ya uhakika ya kuuza mazao yao.

Wajumbe wa baraza la biashara la wilaya ya Karatu wakiwa katika kikao

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa