• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

UKARABATI WA MADAWATI UFANYIKE SHULENI

Posted on: January 25th, 2021

Na Tegemeo Kastus

Madawati, Meza na viti vilivyokuwa vimepelekwa kukarabatiwa na matokeo yake kutelekezwa kwa fundi Seremala kwa muda wa miaka miwili bila kufanyiwa matengenezo vyarudishwa shule ya sekondari Gyekrum Lambo.

Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda baada ya kufanya ziara ya kushitukiza katika kijiji cha G-Lambo kijiweni na kukuta madawati 26 meza 17  na viti 16 vilivyokuwa vimewekwa katika stoo ya fundi Wilbrod Qabi   Hayshi. Viti hivyo vimekaa muda mrefu kutokana na shule ya sekondari G-Lambo kushindwa kukamilisha madai ya  fedha  kiasi cha 12,8000 zilizokuwa zinadaiwa na fundi seremala. Wilbrod Qabi   Hayshi aliyekuwa akikarabati thamani hizo.

Mh. Kayanda amemuelekeza Mkuu wa shule ya sekondari G-lambo kuhakikisha viti meza pamoja  na madawati hayo yanarejeshwa shuleni. Amesema madawati hayo yatengenezwe yakiwa shuleni ndani ya kipindi cha siku kumi na nne na shule ilipe deni fundi seremala Wilbrod Qabi   Hayshi ndani ya kipindi cha siku kumi na nne.

Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ametembelea ujenzi wa vyumba vya madarasa mawili pamoja na ofisi ya walimu katika shule ya Baray Khusumay ujenzi unaojengwa kwa nguvu za wananchi wakishirikiana na serikali ya kijiji. Mh. Kayanda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa madarasa na ameelekeza Halmashauri kuhakikisha inakamailisha upauzi  wa majengo hayo ndani ya mwezi huu.

Mh.Abbas Kayanda (aliye mbele) akikagua ujenzi wa vyumba vya madarasa katika shule ya sekondari Dkt. Wilbroad na Baray Khusumay 

Mh. Kayanda ametembelea pia ujenzi wa vyumba vya madarasa unaojengwa kwa nguvu za wananchi pamoja na serikali ya kijiji katika shule ya sekondari  Dkt. Wilbroad Slaa. Sambamba na kukagua ujenzi  huo Mh. Kayanda ametembelea na kukagua ujenzi wa bweni la wasichana linalojengwa na wafadhili katika shule hiyo. Ameelekeza mafundi kuongeza kasi ya ujenzi ili bweni hilo liweze kukamilika kwa wakati.


Matangazo

  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI September 01, 2023
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa