• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

VIONGOZI WA DINI, TUKEMEE MMOMONYOKO WA MAADILI

Posted on: November 9th, 2020

NA TEGEMEO KASTUS

Viongozi wa dini waombwa kuweka mkazo katika kusimamia maadili ya jamii, ili kupunguza vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia pamoja na upotevu wa maadili ambavyo vimezidi kukithiri katika jamii.

Hayo yamesemwa na mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda wakati akifungua semina ya kamati ya umoja  ya viongozi wa dini inter faith. Amesema serikali ina amini sana viongozi wa dini katika kujenga jamii yenye hofu ya Mungu. Amesema changamoto ya upotevu wa maadili inasababisha watoto kutaabika; na imeongeza watoto wanaoishi katika mazingira magumu, lazima tuwaambie na tuwabadilishe nafsi zao watu hawa, kwamba mambo wanayoyofanya hayampendezi mwenyezi Mungu.

Mkuu wa wilaya ya Karatu, Mh. Abbas Kayanda akizungumza na kamati ya umoja wa viongozi wa dini katika ukumbi wa KKKT Karatu 

Mh. Kayanda amepongeza wazo la kuwa na  kamati ya umoja wa viongozi wa dini (inter face) amesema umoja huo utasaidia serikali katika mazoezi ya kitaifa kama chanjo, kusaidia kuhamasisha wananchi. Umoja wa viongozi wa dini inter face utasadia kuleta wananchi  pamoja. Sambamba  na hayo Mh. Kayanda amewashukuru viongozi wa dini kwa kuombea amani ya nchi kipindi cha uchaguzi. Tumemaliza uchaguzi wetu salama hakuna vita wala hakuna ogomvi hili ni jambo la kujivunia. amesema uchaguzi Mkuu umeisha lazima wananchi tuungane na tuwe kitu kimoja na tushiriki katika shughuli za maendeleo. Maendeleo ya wanakaratu yataletwa na wana karatu wenyewe na si mtu nje ya Karatu.

Mh. Kayanda ameomba viongozi wa dini kuendelea kuhubiri amani na kuitunza, kwa sababu ndio msingi wa maendeleo ya nchi. Amesema amani ni tunu ya kipekee, hatuwezi kujenga hospitali kujenga barabara au kununua ndege kama amani itatetereka. Mh. Kayanda ametumia nafasi hiyo kupongeza kamati ya umoja wa viongozi wa dini inter face  kwa miradi mbalimbali wanayosimamia kwa ajili ya kusaidia jamii.

Akitoa neno la shukrani  Padre Pamphili Nada amesema viongozi wa dini wataendelea kuhubiri amani kwa kundi kubwa la waumini ambalo  liko nyuma yao. Amesema lazima mwanadamu apate maendeleo ya kweli ya roho na mwili, amani ikitoweka basi hakuna kitakachowezekana. Tunashukuru Mungu tumepata Rais makini mwenye maono, ujasiri wake umetuvusha kwenye changamoto ya korona. Viongozi wa dini  kwa pamoja wameahidi kuendelea  kushirikiana na serikali wakati wowote.

Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda akiwa katika picha ya pamoja na kamati ya umoja wa viongozi wa dini  Karatu

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa