• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WAFANYABIASHARA: WALALAMIKIA ELIMU DUNI YA KULIPA KODI

Posted on: June 20th, 2019

Wafanyabishara wa wilaya ya Karatu, wamelalamika mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe. Theresia Mahongo juu ya ushrikishwaji duni wa kodi wanazotozwa katika maeneo yao ya biashara. Wamesema wao hawapingi kulipa kodi ila wanapaswa wajengewe ufahamu wa kulipa kodi hasa katika tozo na kodi mpya zinazoanzishwa.

 Mhe. Theresia Mahongo alikuwa akipokea kero za wafanyabishara wa wilaya ya Karatu katika ukumbi wa Sumawe Complex Karatu. Kikao hicho kililenga kusikiliza na kutafutia ufumbuzi kero  mbalimbali za wafanyabishara ili kutengeneza mazingira rafiki katika shughuli zao za kibiashara. 

wafanyabiashara katika ukumbi wa Sumawe Complex wakifuatilia kwa makini mkutano

Mhe. Theresia amesema kikao cha mwisho walichokaa na wafanyabiashara ilikuwa mwezi wa tatu mwaka huu. Katika kikao hicho wafanyabishara walijadili kuhusu sekta ya kilimo juu ya  gharama za uzalishaji kuwa kubwa kwa sababu ya kukosa elimu stahiki ya kilimo. Mhe. Theresia amesema katika kikao hicho walibaini matatizo ya kutofanya utafiti wa udongo ili kujua viwatilifu stahiki vya kutumia. Amesema haya yamesababishwa na wataalamu wa kilimo kutotimiza wajibu wao vyema katika kuwasaidia wananchi katika shughuli za kilimo.

 Mhe. Theresia amesema katika kikao kilichopita kulikua na swala la elimu duni juu ya uanzishwaji wa viwanda vidogo na vyakati ikiwa pamoja na mtaji. Gharama za pango umeme; gharama za maji, ushuru wa maeneo, ushuru wa mazao, gharama za utupaji taka, malipo kabla ya kuanza kufanya biashara, kuwa makubwa. Kikao hicho kilibaini pia wafanyabashara kukosa mkopo wenye riba nafuu. Katika sekta ya utalii kulikuwa na changamoto ya magari ya utalii kusimamishwa mara kwa mara na askari wa usalama wa barabarani.

Mhe Theresia amesema ili wafanyabiashara wafanye kazi vizuri lazima kuwe na mazingira ya amani. Amesema nchi isiyo na amani hakuna mazingira mazuri ya biashara, Mhe Theresia amesema katika hotel kubwa tayari ameshaelekeza wafanyabishara kufunga kamera za usalama. Mhe. Theresia amewatoa hofu wafanya biashara amesema nchi ina amani hivyo waendelee na biashara zao kama kawaida

Mhe.Theresia amewakumbusha  wafanyabiashara  umuhimu wa kulipa kodi. Amesema kunawatu hawalipi kodi jinsi invyopaswa, amesema hakuna taifa linalojengwa bila wananchi kulipa kodi. Amesema kuchelewa kulipa kodi kwa wakati, kunamsababisha mfanyabiashara kulipa kodi pamoja na  adhabu ya kuchelewesha kulipa kodi kwa wakati (with interest). Amewaomba wafanyabiashara kulipa kodi kwa wakati amesema ana majina ya watu wasiolipa kodi inavyostahili. Mhe. Theresia amemuelekeza meneja wa TRA  wa wilaya kutafuta mfumo rafiki wa kuwapa taarifa za kulipa kodi wafanyabiashara, amesema wanaweza kutumia ujumbe mfupi wa simu kwa wafanyabiashara ili waweze kukumbushwa pindi mda wa kulipa kodi unapofika  Mhe. Theresia ameahidi pia kulipeleka swala la utitiri wa kodi ya misitu sehemu husika ili liweze kutatuliwa. swala hilo ni moja ya kero zilizoibuliwa na wafanyabiashara wa wilaya ya Karatu.                                      

Awali katika kikao hicho mfanyabiashara Peter Masay amelalamikia juu ya utitiri wa kodi katika sekta ya misitu.  Amesema katika biashara yake ya mbao anapata changamoto juu ya kodi nyingi wanazokabiliana nazo katika biashara ya mbao. Ndugu Peter amesema kuna kodi zaidi ya ishirini na moja katika idara ya misitu. Amesema kwenye eneo moja la biashara unalipa kodi, ulipe mashine ya kupasulia, ulipe kodi kwa ajili ya mbao, ulipe kodi ya mabanzi, bado kulipa kodi ya TRA, kuna kulipa kutokana na ulivyochukua mzigo lakini amesema kodi imekuwa haiangali mzunguko wa biashara.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa