• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WAKULIMA WAOMBA KUTAFUTIWA SOKO LA UHAKIKA

Posted on: June 20th, 2019

Wafanyabiashara wamemueleza Mkuu wa wilaya ya Karatu Mhe Theresia Mahongo kwamba soko la mazao ya kilimo limedorora. Kero hizo zimetolewa na wafanyabiashara wa wilaya ya Karatu katika kikao  cha wafanyabiashara kilichowahusisha watendaji mbalimbali wa Halmashauri. kikao kililenga kusikiliza changamoto mbalimbali wanazokabiliana nazo wafanyabiashara katika shughuli zao  za kila siku ili kuwajengea mazingira rafiki ya kufanya biashara.

 Mhe. Thresia Mahongo amesema kuna haja ya kufanya utafiti tena Mang’ola juu ya kupungua uzalishaji wa vitunguu. Mhe. Theresia amesema upo umuhimu wa wakulima pia kufuata maelezo kitaalamu katika kujihusisha na kilimo cha kisasa. Kupuuzia maelelekezo ya kitaalamu katika kufanya shughuli za kilimo kunasababisha uzalishaji wa nafaka  kupungua. Mhe. Theresia Mahongo  amesema swala hilo bado linafanyiwa kazi, ili liweze kupatiwa ufumbuzi wa kina juu ya kupungua uzalishaji wa vitunguu Mang'ola. Mhe. Theresia amesema  amelichukua swala la viwanda vya ndani kukwepa  kununua ngano inayolimwa na wakulima wa ndani jambo linalofanya wakulima wa ngano kukosa soko la uhakika la zao la ngano. Ngano hutumika kutengeneza mikate lakini pia sankisti lakini baadhi ya vinywaji, makapuni ya ndani yamekuwa yakinunua zao hilo kutoka nje ya nchi.


wafanyabiashara wakifuatailia ajenda za kikao kwa makini katika ukumbi wa Sumawe complex Karatu.

Ndugu Paulo Jackobo Afisa bishara wa wilaya amesema kuna udalali mkubwa unaofanywa kwa wakulima wa vitungu Mang’ola wakati wa ununuzi wa vitunguu. hali inayosababisha wakulima kukosa bei nzuri ya vitungu pindi wanapouza. Ndugu Jackobo amesema ujazo sahihi wa gunia ni kilo 100 na siyo zaidi ya hapo lakini wakati wa ununuzi wafanyabishara wanakuja na vifungashio vienye ujazo mkubwa zaidi ya kipimo elekezi. Licha ya elimu kutolewa kwa wakulima juu ya kuepuka kufunga rumbesa ili wasinyonywe na  wachuuzi wakulima wamekuwa wakishirikiana na wafanyabiashara wakati wa uzaji wa vitunguu.  Ndugu Jackobo  Amesema  Halmashauri imejipanga kutuma wataalamu Nairobi Kenya na Uganda ili kukutana na wanunuzi wakubwa wa vitunguu na wawaunganishe moja kwa moja na wakulima wa vitunguu. Lengo likiwa ni kuondoa udalali unaofanywa kwa wakulima wa vitunguu Mang’ola ili waweze kunufaika na kilimo.

Awali ndugu Zakaria  Qamara amemueleza mkuu wa wilaya kwamba  kikundi cha kulima ngano na shairi wanamalengo ya kujenga kiwanda cha ngano na shairi. Lakini kutokana na hali ya hewa kubadilika imefanya mazingira ya uendelezaji wa kilimo kutokuwa rafiki.Amesema watu wameacha kulima ngano kwa sababu hakuna soko zuri linalowanufaisha wakulima. Ngano inatumika kutengenezea sankisti na mikate. 

Ndugu Qamara amesema kuna tatizo la makampuni makubwa kununua ngano kutoka nje ya nchi na kuacha ngano inayolimwa ndani. Wamesema wao kilimo ndio uti wa mgongo, wameomba kupewa elimu nzuri ya kilimo ili waweze kuzalisha ngano yenye ubora. Lakini pia wameomba kuzuia makapuni makubwa kununua ngano kutoka nje na kuiacha ngano inayolimwa Tanzania. Lakini pia amezungumzia swala la Mang’ola namna uzalishaji wa vitunguu ulivyopungua; ndugu Qamara amezungumzia pia soko la Mang’ola la vitunguu ambalo nalo limekosa ufanisi, katika kusaidia wakulima kupata bei nzuri ya zao la vitunguu . Amewaomba wataalamu wa kilimo waweze kusaidia kuboresha uzalishaji kama awali na kupata soko la uhakika la mazao yao.  .

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa