• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WALIMU WA BVR WAPEWA SIKU MOJA OFF

Posted on: July 25th, 2019

Afisa mwandikishaji wa ngazi ya jimbo ndugu Waziri Mourice amewashukuru wafanyakazi walioendesha zoezi la uandikishaji wa maboresho ya daftari la  wapiga kura. Wafanyakazi hao wa muda wamekusanyika Halmashauri kukabidhi vifaa vya BVR, takwimu za uandikishaji kwa maafisa wa tume, pamoja na kupewa stahiki zao.

Ndugu waziri mourice amesema amezunguka vituo 186 kati ya vituo 222 vilivyowekwa kwa ajili ya kujiandikisha, ametembelea Tarafa ya Mbulumbulu, Tarafa ya Eyasi, Tarafa ya Endabash na Tarafa ya Karatu. Amejionea kazi jinsi ilivyofanyika kwa umakini na juhudi kubwa na amejionea na kutatua changamoto mbalimbali zilizojitokeza wakati wa zoezi la uandikishaji.

Ndugu Waziri amesema kuna maeneo mengine yalikuwa na hali ngumu kiutendaji hakuna chakula, barabara ni mbovu lakini bado kazi imefanyika. Amesema kuna maeneno hata ukiwa na fedha huwezi kununua chakula, na maeneo mengine  hata kufanya mawasiliano ya simu haiwezekani. Amewashukuru sana kwa utendaji kazi wao kwa sababu wangeweza kukataa kufanya kazi na kukwamisha zoezi la uandikishaji. Amepongeza watumishi hao pia kwa kuhifadhi vifaa vya BVR KIT kwa usalama mkubwa. Hakuna kifaa kilichoharibika wakati wa zoezi hilo wala kuibiwa jambo ambalo linatoa taswira na sifa nzuri kwa Halmashauri.

BVRT OPERATORS wakikaguliwa vifaa vyao kabla ya kuvikabidhi kwa maafisa wa tume.

Ndugu waziri Mourice amesema ameandika mawasiliano ya watendaji kazi wote ili zoezi jingine likijitokeza wapewe nafasi. Ameshukuru waandikishaji kwa kumpa sifa kubwa kwa kazi nzuri waliyofanya kwenye zoezi la maboresho la wapiga kura. Amesema kwa uungwana waliofanya wamemvisha nguo na kupokea sifa ambazo wao walistahili kuzipata. Amesema  moyo walioonesha katika kazi hiyo ndio uliofanya zoezi kwenda vizuri. Ameongeza kusema kama mwandikishaji au BVR OPERATOR angeaamua kuacha kazi tayari zoezi lingeingia dosari. Amewaomba wafanyakazi hao wa muda kuomba nafasi za kazi  wakati wa uchaguzi wa serikali za mitaa na uchaguzi mkuu mwaka unaokuja. Amewaambia ameshaweka kazi data (data base) ya watu wote waliofanyakazi katika zoezi hilo ili wawape kipaombele.

Ndugu Waziri Mourice amewapa siku moja ya mapumziko walimu wote walioshiriki katika uandikishaji wa zoezi hilo kwa kazi ngumu waliokuwa wakiifanya.Amefanya hivyo kuthamini mchango wao wa kazi katika zoezi hilo. Amewaahidi wafanyakazi wengine ambao si watumishi wa serikali kuwaandikia barua ya udhamini pindi watakapopata ajira sehemu yeyote na wakahitaji mdhamini. Amewaasa kutokata tama katika majukumu yao ya kila siku, amesema kila kitu kinawezekana pindi unapojituma na kuweka nia.

Maafisa waandikishaji wakikabidhi nyaraka mbalimbali Halmashauri  baada ya zoezi la uandikishaji kukamilika.

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa