• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WAFURAHIA KUPATA ARDHI YA UZALISHAJI

Posted on: February 17th, 2021

Na Tegemeo  Kastus

Wananchi wa kijiji cha Mikocheni kata ya Endamaghan wamefurahia kupata ardhi kwa ajili ya kufanya shughuli za uzalishaji. Halmashauri ya kijiji cha Mikocheni iandae utaratibu maalumu wa kuwatambua na kuwagawia wananchi wa kijiji cha Mikocheni ili waweze kujikita katika shughuli za kilimo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda alipofanya mkutano wa hadhara katika kijiji cha mikocheni. Amesema utaratibu uliokuwa unafanywa na Halmashauri ya kijiji cha Mikocheni wa kumpa mwananchi mmoja hekari mia ili aweze kujenga visima vya maji vitatu ni batili. Amesema ameufuta mpango huo na amemuelekeza Afisa Mtendaji kata wa Endamaghan asimamie utaratibu wa kuwatambua na kuwagawia wananchi ardhi, ameongeza kusema ardhi ni mali. Ardhi haiongezeki lakini watu wanaongezeka, unaweza usiwe na uwezo wa kuiendeleza eneo leo lakini kesho ukapata uwezo wa kuliendeleza baaadae.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda akizungumza na wananchi wa Mikocheni.

Katika hatua nyingine Mh. Abbas Kayanda ameelekeza Mkaguzi wa ndani wa Halmashauri pamoja na watu wa RUWASA kuchunguza fedha za iliyokuwa kamati ya maji Mikocheni na Endamaghan inayoitwa (Endamaiko) ili kujiridhisha na mapato  na matumizi. Amesema hayo baada ya wananchi kulalamikia kukosekana kwa uwazi wa mapato na matumizi ya kamati hiyo ya maji.

Naye Afisa Mtendaji kata wa kijiji cha Mikocheni Ndg. Simon Mafie amesema kijiji cha Mikocheni huduma za maji safi na salama zimeathirika kutokana na miundo mbinu duni ya iliyowekwa na {Endamiko}. Amesema hata mradi wa maji wa shirika la world vision umeathirika kufanya kazi kwa sababu eneo walilojenga mashine za kusukumia maji safi na kusambaza kwa wananchi limekumbwa na mafuriko  ya ziwa Eyasi.

Wananchi wakichangia katika mkutano huo wa hadhara Diwani mstaafu wa kata ya Endamaghan Mh. Sophia ameomba wakala wa barabara  vijijini kujenga matoleo ya maji wanapokarabati barabara vijijini. Amesema kujenga barabara bila kuwa na matoleo ya maji kunasababisha maji kutuwama barabarani hivyo kuzidi kuharibu barabara.

Mkuu wa wilaya katika matukio tofauti akizungumza na wananchi wa kijiji cha  Mikocheni 

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • NAFASI ZA KAZI 2024 April 21, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa