• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WANANCHI WAKIMBIENI MAWAKILI VISHOKA

Posted on: February 2nd, 2021

Na Tegemeo Kastus

Wanasheria vishoka wana wanawalagahi wananchi na kuwatoza gharama kubwa za fedha zisizo na msaada wowote wa kisheria. Wananchi wenye mashauri yao mahakamani wanapaswa kupata ushauri na msaaada wa kisheria kwa mawakili wanaotambulika kisheria.

Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Abbas Kayanda amesema hayo katika kilele cha siku ya sheria ya mawakili wanaotambulika na serikali kilichofanyika katika viwanja vya Mahakama ya wilaya ya Karatu. Kauli mbiu ya mwaka huu ni miaka  100 ya  Mahakama kuu, katika kujenga nchi inayozingatia uhuru  haki undugu amani na ustawi wa wananchi 1921- 2021. Amesema wananchi wanapaswa kuleta ushahidi na mashahidi ili shauri liamuliwe mahakamani kwa kuaangalia haki ipo wapi kwa mujibu wa sheria. Kuna kesi mbalimbali ambazo zimefunguliwa lakini hazitolewi ushahidi, mwisho wa siku kesi zinaenda kumalizwa nyumbani.

wananchi wakifuatailia matukio mbalimbali katika  kilele cha siku ya sheria

Mh. Kayanda amesema baraza la ardhi na nyumba  limekuwa na kesi  nyingi za muda mrefu, ametoa rai kwa mwenyekiti wa baraza kuongeza kasi ya kusikiliza migogoro ya ardhi kwa maana kesi zinapochukuwa muda mrefu wananchi wanaanzaa kujenga tafsiri hasi juu ya kesi zao.

Ameomba wapelelezi kuongeza kasi ya uchunguzi wa kesi  wanazopeleleza  ili mashauri yakamilike mapema, amesema kumekuwa na malalamiko juu mahakama wanachi wakilalamika kuchelewa kupata nakala ya hukumu. 

Mh Kayanda amesema wiki ya sheria ilifanyika katika uwanja wa mazingira bora, wiki hiyo ilikuwa  maalumu kwa wananchi kupata msaada wa kisheria bure. Mwaka huu  mwiitikio wa wananchi ulikuwa ni watu 120 ni mwamko mdogo mno. Ametoa rai kwa wananchi siku za usoni kujitokeza katika wiki ya sheria ili kupata msaada wa kisheria.

Akizungumza katika kilele cha sherehe za siku ya Mahakama Hakimu Mkazi mfawidhi wa mahakama ya Karatu Mh. Is-haq Kuppa amesema mahakama imeanza kuendesha mashauri kwa mfumo wa Tehama. Amesema kesi zote zinasajiliwa kwa mfumo wa Tehama na imesaidia kupunguza kesi za nakala za hukumu.

Mh, Abbas Kayanda akiwa katika picha ya pamoja na mawakili 

Mh. Kuppa amesema mahakama ya wilaya yaKaratu ina mashauri 122 amabyo yapo ambazo kituo ina mamlaka nazo ya kumaliza na kesi ambazo mashauri yanazuio, kesi ambazo hawana mamlaka nazo.  Amesema mashauri hayo yamepungua na yako kwa uwiano wa kusikiliza kwa mahakimu watatu.

Mh. Kuppa amesema Karatu hakuna uhaba wa mawakili lakini wananchi wengi wanatumia wanasheria wasio rasmi. Amesema hii inasababisha haki za watu kupotea, kwa sababu mashauri yanakosa mashiko ya ushahidi unaotakiwa kisheria.

Mh, kuppa amesema kumekuwa na kasumba ya watu kufanya mauziano ya maeneo mkataba unaweka chini uthibitisho wa Mahakama. Mh kuppa amesema mahakama haifanyi uthibitisho wa mikataba, amesema hayo ni madhara ya kuandaa mikataba na watu ambo hawana weledi wa taaluma ya sheria.

Matangazo

  • WALIOCHANGULIWA KIDATO CHA KWANZA - 2023, HALMASHAURI YA KARATU December 14, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM PROGRAM NEW ENTRY FEE December 01, 2022
  • TANGAZO LA KUITWA KWENYE USAILI NAFASI YA MTENDAJI WA KIJIJI DARAJA LA 111 NA MSAIDIZI WA KUMBUKUMBU DARAJA LA 11 May 07, 2021
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MIAKA (61) YA UHURU MKUU WA WILAYA YA KARATU MHE DADI HORICE KOLIMBA AFUNGUA MDAHALO WA MAENDELEO WILAYA YA KARATU.

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • MAADHIMISHO YA MIAKA 61 YA UHURU WA TANGANYIKA

    December 09, 2022
  • LAKE EYASI CULTURAL TOURISM TO BE IMPROVED

    November 08, 2022
  • Angalia Zote

Video

NDUGU. EDWARD MAURA MWENYEKITI WA BARAZA LA WAFUGAJI NGORONGORO
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754266833

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa