NA TEGEMEO KASTUS
Jengo la choo cha mnadani lilokuwa limetelekezwa kwa muda mrefu, na miunndo mbinu yake kuharibiwa limekarabatiwa upya. Ukarabati wa maliwato umefanyika baada ya Mkuu wa wilaya kukagua na kutoa maelekezo kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Hlamshauri ya Karatu kukarabati na kuweka walinzi ili wafanyabiashara wapate huduma za maliwato.
Hayo yamebainika baada ya Mkuu wa wilaya a Karatu Mh.Abbas Kayanda pamoja na kamati ya ulinzi na usalama kufanya ukaguzi katika jengo hilo lilopo katika eneo la mnadani Karatu. Ukarabati wa jengo hilo utasaidia wafanyabishara kupata huduma ya maliwato bila kufanya uchafuzi wa mazingira.
Hali ya Jengo la Maliwato jinsi ilivyo sasa baada ya ukarabati mkubwa kufanyika eneo la Mnadani Karatu.
Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ujenzi wa zahanati wa zahanati ya Ngaibara na ametoa maelekezo Mahususi kwa watendaji kuhakikisha ujenzi miundo mbinu ya majengo unakamilika haraka iwezekanavyo. Wakti huo huo Mh. Kayanda ameridhishwa na kasi ya ujenzi wa jamvi katika jengo la maabara unaofanyika kituo cha afya Endabash baada ya kutembelea eneo la ujenzi.
Mh. Abbas Kayanda akikagua mashine mpya zilizoletwa katika kituo cha afya Endabash.
Mh. Kayanda amejionea vifaa vipya vilivyoletwa na Msd kwa katika Kituo cha afya Endabash ikiwemo mashine ya kutunzia watoto wachanga (incubator) mashine kwa ajili ya wagonjwa wa pumu inayosaidia mgonjwa wa pumu kuvuta na kurudi katika hali ya kawaida. Mashine Maalum kwa ajili ya kuchemshia vifaa vya hospitali, kuepusha maambukizi kwa kutumia vifaa lakini pia kuna mashine ya kupimia kipimo kikubwa cha damu.
Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya daraja la barabara.
Mh. Kayanda ametembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa barabara ya mnadani Endabash kuelekea Endamarariek pamoja na ujenzi wa Josho. Miradi yote iliyotembelewa iko katika hali nzuri na ametoa rai kwa viongozi kuzuia kupitisha ngombe kwenye barabara ili kuepusha uharibifu wa barabara. Ameelekeza uongozi wa kijiji kusimamia usafi na kulitunza jengo la mradi wa machinjio ya mnadani Endabash.
Mh. Kayanda ametembelea na kujionea ujenzi wa mradi wa maji kitongoji cha Kansay mradi ambao utasaidia shule ya msingi Haraa kupata maji pamoja na kusambaza huduma ya maji kwa wananchi. Sambamba na mradi huo ametembelea na kujionea maendeleo ya mradi wa maji shule ya msingi Geer ambao umeanza kufanya kazi na kusaidia shule na wanakijiji wa eneo hilo.
Mh. Abbas Kayanda akikagua ujenzi wa miundo mbinu ya Machinjio Mnadani Endabash.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa