• Wasiliana Nasi |
    • Maswali |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Complains |
Karatu District Council
Karatu District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Dhamira na Dira
    • Historia
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Fedha na Biashara
      • Ujenzi
      • Afya
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
    • Vitengo
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
  • Madiwani
  • Miradi
    • TASAF
    • BOOST
  • Machapisho
    • Hali ya Uwekezaji
      • Business License Form
  • Kituo cha Habari
    • Video
    • Habari
    • Hotuba kwa Vyombo vya Habari
    • Maktaba ya Picha

WITO WATOLEWA KWA WANANCHI, KUTUNZA MIUNDO MBINU YA MAJI

Posted on: September 8th, 2020

NA ALICE MAPUNDA

Wananchi wa kata ya Kansay wametakiwa kuilinda na kuitunza miradi ya maji waliyoletewa na serikali ili iwasaidie vizazi hadi vizazi.Maelekezo hayo yametolewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Iddi Hassan Kimanta alipokuwa akikagua na kuzindua miradi ya maji katika Kijiji cha Kansay na Kambi ya Faru, wilayani Karatu.

Amesema zaidi ya milioni 125 zimetolewa katika ujenzi wa mradi wa maji katika Kijiji cha Kansay na milioni 15 katika Kijiji cha Faru ili kuhakikisha miradi hiyo inakamilika na kutoa maji.Kimanta amesema, Serikali ya awamu ya tano inaendelea kuhakikisha inatekeleza kauli mbiu ya “Mtue mama ndoo ya maji” katika maeneo mengi ya nchi ikiwemo wilaya ya Karatu.Mradi wa maji wa Kijiji cha Kansay utawafikia wananchi takribani 4768, shule 3 na kituo cha afya kimoja, wakati katika Kijiji cha kambi ya Faru mradi huo utawafikia wananchi takribani 3500, mifugo 2000 na shule 2.Nae, kaimu mkuu wa kitengo cha wakala wa usambazaji maji na usafi na mazingira vijijini (RUWASA) wilaya ya Karatu Daudi Mwenduganga amesema,miradi hiyo ya maji imeweza kusaidia kupunguza magonjwa ya milipuko katika vijiji hivyo.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Iddi Kimanta (katikati) akikata utepe tayari kwa kuzindua mradi wa maji 

Pia, upatikanaji wa maji umeweza kusaidia kuokoa muda wa wanafunzi wengi katika kutafuta maji na badala yake wanautumia muda huo katika masomo yao.Hali kadharika, faida ya miradi hiyo ya maji imewasaidia wamama kupata muda wa kufanya shughuli nyingine za maendeleo ukilinganisha na kipindi cha nyuma walikuwa wanapoteza muda mwingi katika kutafuta maji kwa umbali umrefu takribani kilometa 6 hadi 8.Mwenyekiti wa kamati ya maji Kijiji cha Kansay bi. Thekla Bayo na mwenyekiti wa Kijiji cha kambi ya Faru bwana Israeli Dafi wamesema, wameishukuru serikali ya awamu ya tano kwa kuwaletea maji baada ya kuangaika zaidi ya miaka 7.Wamesema wapo tayari kushirikiana na wanakijiji kuilinda na kuitunza miradi hiyo ili isiaribiwe.

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, yupo katika ziara ya kikazi katika wilaya ya Karatu ambapo, amekagua miradi mbalimbali ikiwepo ukarabati na ujenzi wa miradi ya maji na hospitali, wilayani humo.



Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh. Iddi Kimanta akikagua miundo mbinu ya Maji katika kijiji cha Kansay

Matangazo

  • Matokeo ya upimaji wa Kitaifa kidoto cha pili January 07, 2024
  • Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Uchaguzi wa Wanafunzi wa kidato cha kwanza, 2024 December 18, 2023
  • Matokeo ya Darasa la Nne January 07, 2024
  • KIKAO CHA BARAZA LA MADIWANI 2024 May 11, 2024
  • Angalia Zote

Taarifa Mpya

  • MAAFISA UANDIKISHAJI WALA KIAPO KARATU

    May 14, 2025
  • DED HOKORORO ASHIRIKI KIKAO CHA ALAT WILAYA YA MERU

    May 15, 2025
  • MADAKTARI BINGWA WA SAMIA AWAMU YA TATU WATUA KARAU

    May 12, 2025
  • KARATU WASAPOTIJUHUDI ZA RAIS SAMIA WATANGAZA UTALII WA NDANI

    May 11, 2025
  • Angalia Zote

Video

DC KOLIMBA ATATUA KERO TARAFA YA EYASI KARATU
Video Zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Fursa za Uwekezaji

Viunganishi Linganifu

  • Tovuti ya Wizara ya Fedha na Mipango
  • Jamvi la Habari
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Serikali
  • Sekretarieti ya Ajira

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Wasiliana Nasi

    Karatu District Council

    Sanduku la Posta: P.O Box 190

    Simu: +255 272970648

    Simu ya Mkononi: 0754773947

    Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa