Na Tegemeo Kastus
Kasi ya umalizijaji ujenzi wa zahanati ya kijiji cha Kilimatembo katika kata ya Rhotia imefika katika hatua za nzuri kukamilika. Zahanati hiyo ambayo ilitengewa kiasi cha million kumi na Halmashauri ya wilaya ya Karatu ikiwa ni pamoja na na fedha za kijiji kiasi cha Milion nne kutoka Halamashauri ya kijiji cha kilimatembo na nguvu kazi za wananchi sasa iko katika hatua za umaliziaji wa ujenzi wa kichomea taka na jengo la choo.
Mh. Kayanda akizungumza na viongozi wa kijiji cha kilimatembo
Hayo yamebainika katika ziara ya Mkuu wa wilaya Mh. Abbas Kayanda wakati alipotembelea kujionea maendeleo ya ujenzi wa zahanati hiyo. Mh. Kayanda amepongeza jitihada zilizofanywa na wananchi pamoja na uongozi wa kijiji kwa usimamizi mzuri wa kazi ya ujenzi unaoendelea. Katika ziara hiyo Mh. Kayanda ameelekeza wakala wa barabara vijijini (Tarura) kuweka kwenye bajeti ya mwaka (2022-2023) ujenzi wa wa daraja katika barabara ya Rhotia-Marar ambayo mwaka huu iko katika mpango wa kuchongwa kwa umbali wa km 1. Amesema ujenzi wa daraja hilo utasaidia usalama wa wanafunzi kuvuka wakati wa kwenda shule lakini pia kusaidia wananchi kupata huduma ya afya katika zahanati ya Kilimatembo.
Mh. Kayanda akikagua ujenzi wa jengo la zahanati ya Kilimatembo.
Mh. Kayanda amesema vifaa vyote vya ujenzi vimeshaletwa katika zahanati hiyo ameelekeza wataalamu mpaka mwanzoni mwa mwezi wa kumi zahanati ianze kufanya kazi. Amemuelekeza Mganga mkuu wa wilaya kuanza kutafuta wafanyakazi wa afya watakaokuja kutoa huduma za afya kwa kwenye zahanati ya Kilimatembo.
Mh. Kayanda ameelekeza wakala wa barabara vijijini kuweka katika bajeti barabara ya kutoka kijiji cha Kilimatembo Mpaka kijiji cha Huduma ili iweze kujengwa na kupanuliwa kurahisisha mawasiliano ya barabara ya kijiji hicho. Akizungumzia kuhusu swala la maji amesema serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Mh. Samia Suluhu Hasani imetoa kiasi cha 2.2 billion kwa Ruwasa kwa ajili ya miradi ya maji ikiwemo kiasi cha million 320 kwa ajili ya uboreshaji wa miundo mbinu ya maji katika kata ya Rhotia. Uboreshaji wa huduma za maji utasaidia maji kusambazwa mpaka kijiji cha Kilimatembo.
Mh. Kayanda katika matukio tofauti katika jengo la zahanati ya Kilimatembo
Katika hatua nyingine Mh. Kayanda ameelekeza shirika la umeme Tanesco (Karatu) kufanya upembuzi yakinifu kwenye miundo mbinu ya umeme ili kubainisha na kurekebisha tatizo la kijiji cha Kilimatembo kukosa nishati ya umeme yenye uwezo wa kuhimili vifaa vya umeme wa manyumbani na mashine za kusagia. Amesema malengo ya serikali kufikia mwaka 2025 ni kusambaza umeme mpaka ngazi ya vitongoji baada ya kumaliza ngazi ya kijiji. Amesema ujenzi wa miundo mbinu ya umeme unatakiwa uwe na faida kwa wananchi kama kuwezesha shughuli za kiuchumi na kusaidia katika miradi ya maendeleo.
Mh. Kayanda amehimiza wananchi walijitokeza katika hadhara hiyo umuhimu wa kujiunga katika vikundi ili kuanzisha mradi wa kutundika mizinga ya nyuki katika maeneo ya fireline ambayo huvamiwa na wanyama pori. Amesema kutundika mizinga ya nyuki mipakani mwa hifadhi ya wanayama inasaidia tembo kutoingia kwenye makazi ya watu lakini inasaidia wananchi kujipatia kipato kutokana na asali wanayorina na kuuza. Amesema mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro imeanzisha ufugaji wa nyuki wa vikundi na tayari vikundi 23 vimeshapewa mizinga kwa ajili ya uanzishaji wa mradi huo. Tayari mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro wanampango wa kujenga kiwanda kwa ajili ya utengenzaji wa asali ambacho kitasaidia kuiongezea asali thamani ya fedha.
Mh. Kayanda akiwa katika ziara ya kukagua miundo mbinu ya ujenzi ya elimu sekondari ya Diego.
Amesema mamlaka imekuwa na ikitumia vijana waliopewa mafunzo (Game scout) ambao wanatoka katika vijiji vinavyozunguka hifadhi ya mamlaka Ngorongoro ili kusaidia kurudisha wanyama wanaoingia kwenye makazi ya watu. Ikiwa na pamoja na kupaka oil chafu na pilipili ambayo inasadia sana wanayama mwitu kutoingia kwenye makazi ya watu, amesema sambamba na hilo vijana hao wanasaidia kutoa taarifa mbalimbali katika vituo vya ulinzi vya hifadhi kusaidia kukabiliana na vitendo vya kijangili
Awali katika ziara hiyo Mh. Abbas Kayanda alitembelea shule ya sekondari Diego na Kilimatembo kujionea hatua za ujenzi wa vyoo katika shule hizo. Mh. Kayanda amehimiza watendaji kuongeza nguvu kazi ili miradi ya ujenzi wa vyoo katika shule hizo ili viweze kukamilika kwa wakati. Ujenzi wa wa matundu ya vyoo uko katika hatua za mwisho na kilichaobaki ni ukarabati wa mdogo mdogo ambao uko katika hatua nzuri.
Picha katia matukio tofauti wakati wa ziara ya kukagua miundo mbinu ya elimu katika shule ya sekondari Kilimatembo.
Karatu District Council
Sanduku la Posta: P.O Box 190
Simu: +255 272970648
Simu ya Mkononi: 0754773947
Barua Pepe: ded@karatudc.go.tz
Haki Miliki @ 2017 Halmashauri ya Wilaya ya Karatu.Haki zote zimehifadhiwa